MAHAKAMA YAAMURU KUKAMATWA KWA RAIS

MAHAKAMA
MAHAKAMA Kuu ya nchini Panama, imeamuru kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Ricardo Martinelli (pichani chini), aliyeongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka sita kuanzia 2009.

Sababu ya amri hiyo ni kutokana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya kutumia fedha za umma kinyume na utaratibu akiwa madarakani ili kufanya upelelezi kwa takriban watu 150 maarufu nchini mwake.

Miongoni mwa waliodaiwa kudhurika na upelelezi huo uliofanyika kinyume cha sheria ni pamoja na wafanyabiashara, wanasiasa, wanasheria, madaktari pamoja na wanachama wa umoja wanaharakati wafanyabiashara.

Ricardo Martinelli 
Hata hivyo, Rais mstaafu Martinelli alikana mashitaka hayo kwa kusema kuwa ni moja ya njama za kumchafua zinazofanywa na Rais wa nchi hiyo aliyeko madarakani, Juan Carlos Varela.

Taarifa zinasema Mahakama imefi kia uamuzi wa kumkamata Martinelli baada ya kushindwa kutokea mahakamani mwanzoni mwa mwezi huu, kwa ajili ya shauri la kwanza.

Kutokujitokeza kwake mahakamani kunasemekana ni kwa makusudi kwa kuwa anaishi mji wa karibu na mahakama hiyo jimbo la Miami.
Previous Post Next Post