KAGASHEKI ALIJIA JUU GAZETI HILI KWA KUMSEMA UWONGO JK

Hamis Kagasheki
WAZIRI wa zamani wa maliasili na utalii, Balozi Hamis Kagasheki ameibuka na kulijia juu gazeti la Raia Mwema kutokana na taarifa yake iliyobeba kichwa cha Magufuli awatia kiwewe CCM ambapo ndani yake iliandikwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dr Kikwete anang’ang’ania kuendelea kuwa mwenyekiti wa CCM ili asimpe nafasi Magufuli kufanya kazi yake vizuri.

Kagasheki amesema kuwa jambo hilo sio la kweli hata kidogo huku akiweka wazi kuwa JK bado hata hajafika kipindi ambacho watangulizi wake walikaa madarakani kama wenyeviti wa chama hivyo amelitaka gazeti hilo na watu wenye mtazamo kama huo kuachana mara moja na suala hilo kwa sababu halina ukweli wowote.
Previous Post Next Post