Chege amesimulia changamoto kubwa iliyompata wakati akishoot video ya wimbo wake Sweety Sweety nchini Afrika Kusini na director Justin Campos.
Chege ameiambia Bongo5 kuwa moja ya changamoto kubwa iliyomkuta ni kupata maumivu ya kiuno hali ambayo ilisababisha kusitishwa kwa shughuli hiyo.
“Kuna ile short ya kwanza kabisa nilipata tatizo la maumivu ya kiuno, kilikuwa kinauma sana ikabidi tupumzike na director akanipa dawa,” amesema.
“Lakini nashukuru Mungu baada ya muda fulani kikapoa na kuendelea na kazi. Director aliambia tatizo ni mawazo ndiyo kitu ambacho kilisababisha tatizo hilo,” ameongeza.
Katika hatua nyingine Chege amesema wimbo Sweety Sweety ndio wimbo wake uliopata mapokezi makubwa kuliko nyingine. Amewashirikisha Runtown (Nigeria) na Uhuru (Afrika Kusini).

Tags
HABARI ZA WASANII