Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika.
Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.
“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi sifa zake,” alisema Nape.
Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015.
Sehemu ya wabunge wa CCM walioshiriki kwenye kikao maalum cha uchaguzi wa Spika kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.
KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndugu ABDULRAHMAN KINANA amefungua kikao cha kamati ya wabunge wa CCM huku akiwahimiza wabunge hao kufanya kazi ili kutekeleza kauli mbiu ya rais dr JOHN MAGUFULI ya hapa kazi tu.
Akifungua kikao hicho leo mjini Dodoma ndugu KINANA amesema ili kuendana na kauli mbiu hiyo nilazima wabunge wote wafanye kazi.
Amesema kazi waliyonayo kwa sasa ni kuwazungukia watanzania ambao wamewaamini kwa kuwa njia pekee ya kutafsiri imani hiyo ni kuwatumikia kwa nguvu zote.
Ndugu KINANA amewapongeza wabunge hao kwa kutafuta kura nyingi za rais juhudi ambayo imekiletea chama heshima kubwa na kuwahakikishia kuwa ofisi yake itaandaa siku maalum kabla ya bunge linalofuata ili kuwapa majukumu ya namna ya kuwatumikia wananchi.
Amesema kazi kubwa kwa wanasiasa ni kutekeleza ilani ya uchaguzi waliyonayo kazi ambayo ana imani kuwa wabunge hao wataitekeleza ipasavyo.
Awali akimkaribisha katibu mkuu,katibu wa wabunge wa CCM mama JENISTA MUHAGAMA amesema kikao hicho nimaalum kwa ajili ya kuchagua jina moja la atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania kutoka katika majina matatu yaliyopitishwa na kamati kuu ya halmashauri ya CCM jana.
Majina hayo yaliyopitishwa ni la naibu spika mstaafu JOB NDUGAI,mbunge wa Afrika Mashariki ABDULLAH ALLY MWINYI na naibu mwanasheria mkuu wa serikali TULIA ACKSON MWASANSU ambaye ameteuliwa na rais kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Tanzania.
Uchaguzi huo unasimamiwa na wajumbe wa kamati kuu ya CCM ambao ndugu WILLIAM LUKUVI,MAUA DAFTARI na JERRY SILAA ambapo jina moja litakalopatikana litapelekwa kesho bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote.
SHUKRANI
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru watanzania kwa imani kubwa waliyoionyesha katika uchaguzi mkuu uliopita uliowezesha kuwapa ushindi wabunge wa chama hicho kwa asilimia 74.8.
Akifungua kikao cha kamati cha wabunge wa CCM kilichofanyika ukumbi wa white house mjini Dodoma katibu mkuu wa chama hicho ndugu ABDULRAHMAN KINANA amesema kitendo hicho kimedhihirisha imani kubwa waliyonayo watanzania kwa CCM.
Amesema watanzania wametafsiri imani kwa kukipa kura CCM na kusema katika majimbo tisa yanayofanya uchaguzi mdogo tayari CCM imeshinda katika jimbo la Lulindi lililopo mkoani Tanga.
Aidha amesema katika kata 14 zilizofanya uchaguzi mdogo katika jimbo hilo CCM imepata kata 10 na upinzani kata 4.