Kocha wa klabu ya Manchester United, Louis Van Gaal anaona hapo baadaye kuwa mchezaji Anthony Martial ataongoza safu ya mashambulizi katika siku za usoni.
Mchezaji huyo wa miaka 19, aliyesajiliwa kutoka klabu ya Monaco kwa pauni milioni 36, mnamo mwezi Agosti, amefunga mabao matano msimu huu, lakini amekuwa akichezeshwa upande wa kushoto, ikiwemo mechi ya Jumanne dhidi ya CSKA Mosco.
Louis Van Gaal amesema “ni kijana mdogo sana, lakini ni bora iwapo ataimarika kama mshambuliaji.”
Louis Van Gaal amesema “ni kijana mdogo sana, lakini ni bora iwapo ataimarika kama mshambuliaji.”
Source: BBC