Mkutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Waandishi wa Habari kuhusu zoezi la ubomoaji wa nyumba Manispaa ya Kinondoni (kuanzia kushoto) Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Baraka Mkuya, Kamishna wa Ardhi Tanzania Dkt. Moses Kusiluka na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Bw. Methew Nhonge.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI
Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i. Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini
yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa
shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya
Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika
maeneo yao.
Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.
Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
a) Bila kibali cha ujenzi
b) Bila kufuata michoro ya mipango miji
c) Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.