NIJUZE NIJUZE Author
Title: RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA MBETTE KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA  TEKNOLOJIA TAARIFA KWA UMMA  UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA  TEKNOLOJIA

TAARIFA KWA UMMA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha miaka miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015. 

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka 1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili 2005 hadi tarehe 13 Aprili 2015. 

Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria, TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu cha London, Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu. 

Pia ameshirikiana na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika katika maeneo ya uhandisi, utafiti, TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida mbali mbali.
Imetolewa na:


KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

About Author

Advertisement

 
Top