Dkt Magufuli ampokea TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa Tarehe 5/11/2015.
TB Joshua Kiongozi wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es salaam leo tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Kikwete