Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanne wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Geita Alphonce Mawazo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema chanzo cha tukio ni kwamba kulikuwa na mkutano wa ndani ya chama cha chadema uliofanyika ukumbi wa ludete b ulikuwa unahusu mambo yao ya uchaguzi na walipokuwa wanaendelea katika kikao chao kuna mtu ambaye anadaiwa ni mfuasi wa chadema na kumnong’oneza Marehemu mawazo na baada ya hapo wajumbe walipata mshutuko na kutoka nje na wakakutana na kundi la watu na mtafaruki ulianzia hapo.
Ameongeza kuwa tatizo hilo kutokea kunahusishwa pia na itikadi za kisiasa lakini bado jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake.
Hata hivyo Kamanda Mponjoli amesema hali ni nzuri maeneo ya katoro hasa kata ya ludete ambapo uchaguzi wa diwani umefanyika.
Kifo cha marehemu Mawazo kimetokea jumamosi hii Novemba 14 majira ya saa sita mchana baada ya kuvamiwa na kundi la watu na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi.