Na.Ahmad Mmow. Lindi
Baraza la ushauri la CHADEMA mkoa wa Lindi lilofanya kikao chake kijijini Mtama wiki iliyopita limemkaimisha Selemani Methew Lowongo, kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa Lindi.
Baraza la ushauri la CHADEMA mkoa wa Lindi lilofanya kikao chake kijijini Mtama wiki iliyopita limemkaimisha Selemani Methew Lowongo, kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa Lindi.
Selemani Methew Lowongo (Kushoto) Akipokea Kadi ya Uanachama alipojiunga na Chama cha Chadema.
Lowongo mchezaji wazamani wa timu za Simba na Yanga, ambaye aligombea ubunge katika jimbo la Mtama katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita, alipitishwa na baraza hilo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa chama wa mkoa, Ally Chitanda aliyejiunga na CCM.
Katibu wa CHADEMA mkoa wa Lindi, Mohamed Mahadhi alithibitisha kuwa Lowongo alikaimishwa mwanzoni mwa wiki hii na wajumbe 59 waliohudhuria baraza hilo kutoka wilaya za Ruangwa, Kilwa, Nachingwea, Lindi na Kilwa.
Alisema baada ya kuondoka Chitanda ambaye sasa nidiwani wa kata ya Nangowe wilayani Nachingwea, nafasi hiyo ilikuwa wazi.
"Baada ya Chitanda kukihama chama na kujiunga na CCM nafasi hiyo ilikuwa wazi. Baraza liliona ana uwezo wa kukiongoza, kukijenga na kukieneza chama" Baraza limeona anaimudu nafasi hiyo na atakaimu hadi utakapofanyika uchaguzi," alisema Mohamed.
Alisema kikao hicho ambacho kilikuwa cha kufanya tathimini ya uchaguzi uliopita kilibaini sababu mbalimbali zilizosababisha kutofanya vizuri kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita. Alizitaja sababu hizo kuwa ni viongozi wa kanda, wilaya na mkoa kutokwenda vijijini mara kwa mara.
Sababu nyingine iliyotajwa na katibu huyo ni tangazo la kuachiana maeneo kwa wagombea wa vyama vilivyounda UKAWA kuchelewa. Alibainisha kuwa tangazo hilo lilitolewa wakati wagombea wa vyama hivyo walishafanya maandalizi na kutumia gharama zao.
Hivyo ilikuwa vigumu wagombea hao kuachiana, na kusabisha CCM kushinda nafasi za ubunge na udiwani katika baadhi ya maeneo. Vilevile katibu huyo alisema kikao hicho pia kilibaini chama hicho kimeenea katika mkoa huu.
Kwa madai kwamba kimeweza kupata madaiwani kwenye baadhi ya kata. Huku akitoa pongezi kwa makao makuu ya chama hicho kwa kumteua Latifa Chande, ambaye anatokea mkoa huu, kuwa mbunge wa viti maalum.
Kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita, Luwongo alishindwa kwa takribani kura 13000 alizopata dhidi ya mbunge mteule wa jimbo hilo, Nape Nnauye(CCM) aliyepata kura takribani 18000. Ambapo Isihaka Mchinjita wa CUF alipata kura 10000.