NIJUZE NIJUZE Author
Title: MGOMBEA ALIYESHINDWA UCHAGUZI JIMBO LA MTAMA AZUNGUMZA HAYA KWA MARA YA KWANZA, SABABU ZA KUSHINDWA KWAKE
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mgombea aliyeshindwa Kinyang'anyiro cha Ubunge katika Jimbo la Mtama Mkoani lindi Kupitia chama cha Wananchi (C.U.F) Ndg Isihaka R. Mch...
Mgombea aliyeshindwa Kinyang'anyiro cha Ubunge katika Jimbo la Mtama Mkoani lindi Kupitia chama cha Wananchi (C.U.F) Ndg Isihaka R. Mchinjita ameweza kuzungumza kwa mara ya Kwanza tangu kushindwa kwake nafasi hiyo ya Ubunge.

Mchinjita ametumia fursa hiyo kueleza nini kilitokea hadi kusababisha kushindwa kwake na pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru wapigakura wake na kuwaahidi bado hajakata tamaa.
Isihaka R. Mchinjita
Isihaka R. Mchinjita Akipiga kura wakati wa Uchaguzi mkuu 25/10/2015.

Mchinjita aliyasema haya "Ndugu zangu napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyote mlioniunga mkono wakati wa jitihada za kugombea ubunge jimbo la Mtama kupitia chama changu chama cha wananchi CUF.

Pamoja na kura kuwa hazikutosha kunifanya niwe Mbunge lakini nathamini na kutambua idadi kubwa ya Wana Mtama ambao waliniunga mkono na kujenga matarajio makubwa kwangu. Nawaahidi Hao wote kuwa bado nitaheshimu Imani Yao kwangu na kamwe sitowaangusha.

Aidha Nawapa moyo kuwa nguvu kubwa iliyotumika pengine kuzima matarajio yenu na kujaribu kukatisha tamaa ya dhamira yangu haijafua dafu na hivyo mapambano yanaendelea mpaka tuupate ukombozi wa kweli Wana Mtama .

Naendelea kusisitiza kwamba tareh 25 tulikwenda kuchagua Mbunge wa Mtama na hivyo matokeo ya maamuzi ya tarehe 25 yanamuhusu kila Mwana Mtama bila kujali itikadi ya chama chake.mimi naamini kuwa maoni ya wananchi yalihujumiwa kwa vitisho, Mbinu za kifreemanson zilizotumiwa na maafisa usalama kwa lengo la kugawanya kura za wapenda mabadiliko na ulaghai wa kutumia fedha uliosimamiwa na Mgombea wa CCM huku Takukuru walishindwa kuchukua hatua.

Hata hivyo haya yote yameweza kufua dafu kutokana na uchanga wa Siasa za upinzani jimboni Mtama. Hata hivyo naamini kuwa uchanga huu sasa umetoa fursa ya kujiimarisha kwa kuwa sasa tuna vijiji 21 jimboni,Kata 7 na vitongoji 119.

Natumia fursa hii kuwapa moyo wa ujasiri Wana Mtama wote kuwa safari ya mabadiliko jimboni Mtama imeiva na hatupaswi kurudi nyuma.

I.R.Mchinjita

About Author

Advertisement

 
Top