NIJUZE NIJUZE Author
Title: KIJIJINI KWA MAJALIWA KWALIPUKA SHANGWE BAADA YA KUUKWAA UWAZIRI MKUU, NDUGU NA MWALIMU WAKE WAMUELEZEA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu wa Tanzania awamu ya Tano Ndg: Kassimu Majaliwa (MB Ruangwa) Na.Ahmad Mmow, Ruangwa. Uteuzi wa mbunge wa jimbo la Ruan...
Kassimu Majaliwa

Waziri Mkuu wa Tanzania awamu ya Tano Ndg: Kassimu Majaliwa (MB Ruangwa)

Na.Ahmad Mmow, Ruangwa.
Uteuzi wa mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa awamu ya tano, umeibua nderemo na shangwe kwa wananchi wa kijiji alichozaliwa cha Nandagara kilichopo kata ya Nandagara,wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Lindiyetu.Com ilifunga safari hadi kijijini hapo baada tu ya jina la Majaliwa kutangazwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo nyeti serikalini.
Mwandishi wetu alishuhudia shangwe na shamrashamra kwa wananchi wa kijiji hicho ikiwamo jamaa na ndugu zake waziri mkuu mwenye watoto wanne (Rehema, Saidi, Majaliwa na Zulehika) mume wa Mariam Mbawala.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Lindiyetu.Com walimuelezea Majaliwa kuwa ni mtu wa kawaida anayeweza kuzungumza na mtu yeyote, mtu asiye na majivuno.


Kassimu Majaliwa
MBUNGE wa jimbo la Ruangwa pia Waziri Mkuu wa Tanzania wa Serekali ya Awamu ya Tano Ndg. Kasimu Majaliwa akizungumza na mpigakura wake alipotembelea jimboni mwake hivi karibuni.

Huku wakisema alionekana kuwa na kipawa cha uongozi akiwa tangu mdogo. Baba mdogo wa waziri mkuu huyo, mzee Saidi Hanga ambaye alisema Majaliwa aliyezaliwa mwaka 1960 katika kijiji hicho kitongoji cha Nanditi (Lideko) alikuwa msikivu, mdadisi na mwenye busara asiyependa shari.

Alisema katika maisha yake hakupata kusikia au kuletewa malalamiko kutoka kwa majirani au watoto wenzake kuwa amemtukana mtu au kupigana shuleni nawanafunzi wenzake au mtaani.

Bali alikuwa ni miongoni mwa watoto wakupigiwa mfano wa tabia njema.
"Nimeishi nae na nimetambua tangu akiwa mdogo, tabia yake haikubadilika hata alipopata madaraka" akija hapa hachagui chakula, tunakula sahani moja chakula tulichonacho kama ugali wa muhogo kwa kisamvu anakula tu,"alisema mzee Hanga.

Kuhusu furaha ya kuteuliwa, mzee huyo alisema alijawa nafuraha na hakujisikia hata hamu ya kula baada ya kupata taarifa ya uteuzi wa mwanawe huyo. 

Dada mkubwa wa Majaliwa anayetambulika kwa jina la Esha Hamis Majaliwa, alianza kumuelezea kuhusu maisha yake ya ukiwa aliyokutana nayo baada na mama yake mzazi Majaliwa, marehemu Binasa Issa Chikawe, ambaye alikuwa ni mke mdogo wa marehemu baba yake aliyefariki miaka ya 90, mzee Hamis Majaliwa Hanga.

Alisema Majaliwa aliyesoma shule ya msingi Mnacho na kukulia kijijini hapo kabla ya kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Alisema kaka yake huyo ambaye ni miongoni mwa watoto nane wa marehemu mzee Hamisi alifiwa na mama yake mzazi akiwa mdogo nakufanya amtambue sana baba yake ambaye hakutaka wanawe watoto wake ambao alizaa na marehemu Binasa waende popote baada ya kufiwa na mama yao huyo, bali aliendelea kuishi nao.

Wakiwamo wadogo zake Kassimu. Ambao ni marehemu Suedi aliyefariki mwaka jana na Hamis. Alisema aliishi kwa malezi ya ushirikiano na ndugu wa baba yake akiwa dada yake ambaye ni shangazi wa Kassim. Alimuelezea kuwa alikuwa ni mtoto aliyekuwa na nidhamu na ucheshi uliotanguliwa na upole.


Kassimu Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi Ndg. Kassimu Majaliwa akiongea katika Moja ya Vikao alipokuwa na wadhifa wa Unaibu waziri wa TAMISEMI wilayani Ruangwa.

Tabia ambazo ameendelea kuwa nazo hadi sasa.
"Hana ubaguzi kwa sisi ndugu zake, anakuja hadi hapa na alikuwa anakula chochote anachopewa, nkali ugali gwa ntandaya na nchambula, liponda mbelemende nkali malenga anaweza tauna(hata ugali wa muhogo kwa mboga za majani,kisamvu,mbaazi na hata mihogo mikavu anaweza kutafuna)," alisema Esha ambaye wamezaliwa kwa baba mmoja.

Mpwa wa Majaliwa, Zaudia Mpinda alisema mjomba wake huyo anasifa ya ucheshi nasiyo mbaguzi. Akibainisha kuwa amekuwa msaada kwa ndugu bila ubaguzi, huku akiungana na maelezo ya mzee Saidi na bibi Esha kuwa hakuwa anachagua vyakula hata alipokuwa naibu waziri.

Bali alikula chochote kilichopelekwa mbele yake. Nikutokana na mfumo huo wa maisha hakuwa na mpishi wala mtumishi wa ndani bali alipikiwa na yeye na ndugu zake wengine waliopo kijijini hapo, ikiwamo mke wa mtoto wa baba yake mdogo aitwae Sofia Lyuba ambao wanaishi jirani na ilipo nyumba ya waziri mkuu huyo mpya.

Mmoja wa wananafunzi aliosoma nae shule ya msingi Mnacho, Saidi Makololo alimtaja waziri mkuu kuwa alikuwa na tabia njema shuleni na nyumbani aliyekuwa na tamaa ya maendeleo yasiyo na uchoyo.

Alisema alikuwa mwenye juhudi ya masomo kiasi cha kuwahimiza wanafunzi wenzake wafanye bidii katika masomo.

Sifa nyingine aliyoitaja nikuwa alikuwa mpenda michezo hasa mpira wa miguu. Nakuongeza kusema kuwa tabia njema aliyokuwa nayo ilisababisha walimu wampende na kumtaka waishi nae.

Mwalimu wa Majaliwa anamzungumzia: Mmoja wa wawalimu waliomfundisha katika shule ya msingi Mnacho, mwalimu mstahafu Athuman Mchopa anasema suala la mwanafunzi wake huyo aliyemfundisha kuanzia darasa la tatu hadi la saba na ambaye aliishinae kama mwanawe kwenye nyumba yake katika kipindi chote hicho, alisema kipaji cha uongozi alikionesha tangu akiwa mdogo.

Kutoka na nidhamu, usikivu na juhudi za kujifunza alizokuwa nazo. Nikutokana tabia hizo yeye na walimu wenzake walimuamini na kuwa msaada mkubwa kwao.
"Nilimchukua na kuishi nae baada ya kumuomba mzazi wake, kubwa lililofanya ni mpende ni kunielewa nilichokuwa namfundisha, hivyo alikuwa kama rafiki yangu" nikweli aliweza kuiga hata tabia yangu ya kupenda usafi, nilimfanya kuwa kiongozi wa bendi ya shule na alikuwa anapiga filimbi vizuri sana".

Mwalimu Mchopa alitaja sifa nyingine ya waziri mkuu huyo kuwa ni mpenda michezo. Hasa mpira wa miguu, ambayo yeye alikuwa anafundisha sambamba na bendi ya shule. 

Katibu wa CCM wa kata ya Nandara,Osca Maokola, alisema kuteuliwa kwa nafasi hiyo siyo jambo la kushangaza kwa namna anavyomfahamu.

Maokola ambaye alisema alianza kumfahamu akiwa katibu wa chama cha walimu (CWT) wilaya Ruangwa. Kwamba Majaliwa ataimudu na kuitendea haki nafasi hiyo. Kwa madai kwamba alipokuwa katibu wa CWT alifanya mambo mengi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa ofisi ya chama cha walimu wilaya Ruangwa.

Katibu huyo aliitaja sifa nyingine ni kutokuwa na ubaguzi unaotokana na itikadi za vyama vya siasa."Ingawa ni mwanachama mwenzetu wa CCM lakini hakuwahi kuwachukia wapinzani, daima alikuwa anasema wapinzani nikama marafiki wa maendeleo na demokrasi ndio wanaoisukuma serikali ifanye vizuri kwahiyo sio maadui"

Alisema kutokana na msimamo huo atakuwa kiongozi mzuri kwa vyama vyote, kwani ni msimamo aliokuwa nao kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya juu kiutawala. 

Kassim Majaliwa ni mtoto wa sita kwa baba mzee Hamis Majaliwa. Licha ya waziri mkuu huyo lakini pia marehemu mzee Hamisi alikuwa na watoto wengine ambao ni Seif, Hakika, Said, Fatuma, Esha, Hamis na Bakari.

Pia anae shangazi yake ambaye anatajwa kuwa nimiongoni mwa walioshiriki malezi yake baada ya kufiwa na mama yake. Anayetambulika kwa jina la Sharifa Hanga.

About Author

Advertisement

 
Top