Samatta amesema inaumiza sana pale anapoingia wanjani kutafuta ushindi lakini mambo yanakuwa tofauti na vile anavyotarajia huku kukiwa na idadi kubwa ya watu wanatumaini mazuri huku wakitoa sapoti yao kwa kila hali.
“Matokeo yalikuwa mabaya sana, wote yametuumiza, na inauma sana unapokuwa uwanjani ukijitahidi kufanya kila liwezekanalo lakini mambo hayaendi sawa na huku ukijua kuna mamilioni ya watu wanaotumaini mazuri yafanyike na wanatoa sapoti yao”, Samatta ameandika kwenye account yake ya facebook.
“Kushindwa michuano ni sawa na unaposhindwa vita, unaweza ukaamua kukata tamaa kabisa na kufia uwanja wa mapanbano au unaweza kukubali kushindwa kabla matumaini hayajafa uka-retreat ili ujipange upya”.
“Mimi naiamini option ya pili ndio option ambayo inafanya ndoto ziendelee kuishi na maisha yaendelee. Ninameza maumivu na kuendelea na safari japo hayatokata kiu ila muhimu ni kupita kwenye kipindi kigumu kama hiki. Kushindwa sio silaha ya kutokomeza imani, ila ni teke linalompa maumivu chura na kumfanya atafute njia nyingine ya kupita mpaka afike safari yake”.