Baadhi ya Nyumba zikibomolewa mapema leo mchana mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni,ambapo zoezi hilo linafanyika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo.
Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, imekusudia kuanza kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Baadhi ya wakaazi wa mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni wakishuhudia bomoa bomoa inayofanyika leo katika manispaa hiyo maeneo mbali mbali ambapo Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
Moja ya Nyumba iliyojengwa eneo la wazi katika mtaa wa Bwawani ikibomolewa.
Ubomoaji wa nyumba ukiendelea eneo la Manispaa ya Kinondoni