Dkt. Tulia Ackson Mwansasu
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limempitisha Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge la Tano, kwa kura 250 sawa na 71.2% dhidi ya mpinzani wake, Mh. Magdalena Sakaya aliepata kura 101 sawa na 28.8%.
KABLA YA KUPATIKANA KWA NAIBUSPIKA BUNGE LILIFANYA NCHAKATO WA KUMPATA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.