NIJUZE NIJUZE Author
Title: ZARI AMVUA "DAWA" TIFFAH MKONONI, JE AMESHINDWA KUHESHIMU MILA ZA DIAMOND?
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
DIAMOND upoo! Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ‘hirizi...
DIAMOND upoo! Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ‘hirizi’, hali iliyowafanya watu wengi wabaki na vingi viulizo.
Tiffah
Mtoto wa staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platinumz, Tiffah.

Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyo siku chache baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa mila za Kibongo siyo tatizo.
Hata hivyo, wakati Diamond akitoa ufafanuzi huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ‘hirizi’ hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina, Zari alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye aliyefanya zoezi hilo.
Baada ya Tiffah kudumu na ‘dawa’ hiyo kwa miezi michache (kitu ambacho si cha kawaida), Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na mzazi mwenzake na kuamua kuivua ‘hirizi’ hiyo.
Tiffah
Tiffah akiwa na wazazi wake.
Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana kwenye picha za hivi karibuni alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ‘hirizi’ hiyo na nyingine hana.
Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya Wabongo walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda kuwa alichokifanya siyo sawa.
“Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake, alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambo hayo hayapo. Kitendo cha yeye kwenda Sauzi na kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau, amemdharau Diamond na mama yake pia, siyo sawa,” alisema shabiki wa Diamond aliyejitambulisha kwa jina la Mariam.

Diamond hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake huyo.

About Author

Advertisement

 
Top