Unknown Unknown Author
Title: DIAMOND Vs JAY-Z, TIFFAH NA BLUE IVY WAVUNJA REKODI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mastaa na shoo za ‘kiprofesheno’ SEAN Carter ‘Jay-Z’ ni jina kubwa sana duniani kufuatia mchango wa msanii huyo katika gemu la muziki wa ...
Mastaa na shoo za ‘kiprofesheno’ SEAN Carter ‘Jay-Z’ ni jina kubwa sana duniani kufuatia mchango wa msanii huyo katika gemu la muziki wa Hip Hop. Kupitia umaarufu wa jina lake, umeweza kumpatia mafanikio makubwa na hata kumsaidia mwanaye, Blue Ivy Carter kuvunja rekodi akiwa bado tumboni kwa mamaye siku chache tu baada ya kuzaliwa.
Jay-Z
Jambo hilo lililotokea kwa Jay-Z ndilo limetokea pia kwa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pamoja na mwanaye Tiffah. Katika makala haya yanachambua baadhi ya vitu vinavyoshabiiana kati ya mastaa hao;

Jay-Z na Blue Ivy Historia ya msanii huyu imekuwa ikiwavutia wengi kutokana na jinsi alivyoanza kazi yake ya muziki akiuza CD mkononi kutokana na kukosa msimamizi mpaka mwaka 1996 alipoachia albamu yake ya kwanza iitwayo Reasonable Dought iliyofanya vizuri.

Kwa upande wa ujasiriamali na uwekezaji, anamiliki Klabu 40/40, ni mhisani katika kampuni ya nguo za Rocawear, mdau katika Studio ya Roc- A-Fella na mmiliki wa Kampuni ya Roc Nation.

Kwa upande wa mwanaye, Blue Ivy aliyemzaa na mwanamuziki wa R&B, Beyonce Knowles alianza kuvunja rekodi kabla hata hajazaliwa baada ya mamaye kutangaza kuwa ana ujauzito kwenye Tamasha la Ugawaji Tuzo za MTV mwaka 2011 ambapo ndani ya sekunde moja zaidi ya watu 8,868 walishare taarifa hiyo.

Blue Ivy alivunja rekodi nyingine baada ya kuzaliwa kwa kutajwa kuwa mwanamuziki mdogo kuwahi kutokea kwenye Chati za Billboard kwa kushirikishwa kwenye wimbo wa baba yake uitwao Glory. 
Mbali na rekodi hizo mtoto huyo mwenye miaka mitatu kwa sasa amepata dili kwenye makampuni mengi ya mavazi, ameshirikishwa kwenye nyimbo kadhaa za wazazi wake na inasemekana ndiye mtoto maarufu zaidi duniani.
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz na Princesses Tiffah pia ana historia ya kuvutia ambapo mwaka 2009 alitoa Wimbo wa Nenda Kamwambie kisha mwaka 2010 kuvunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuchukua tuzo tatu za Kili Music.

Diamond amewahi pia kuvunja rekodi kwa kuwa msanii wa kwanza kuuza zaidi ya kopi 1,200,000 za albamu na msanii wa kwanza kufanya shoo iliyoitwa Diamond are Forever na kuuza zaidi ya tiketi 1,500 kwa kiingilio cha Sh. 50,000.

Mbali na tuzo nyingi alizochukua, Diamond amewahi kuwa balozi wa makampuni mengi nchini ikiwemo Coca Cola.

Kwa upande wa bintiye Tiffah, mbali na kupata umaarufu tu akiwa tumboni mwa mama yake Zarinah Hassan, alianza kuvunja rekodi ya kwanza kwa kupata zaidi ya wafuasi 2,000 kwenye ukurasa wake wa Instagram chini ya saa 24 tangu kuzaliwa kwake. 

Lakini pia hadi anafanya sherehe ya kutimiza siku 40, tayari kwenye ukurasa huo alikuwa na wafuasi 126,000 ambao umemfanya kuwazidi baadhi ya mastaa nchini.

Mbali na kuvunja rekodi hizo ambazo hazijawahi kuwekwa na mtoto yeyote yule wa staa Bongo, Tiffah pia ni balozi wa Pugu Mall na Msasani City Mall kwa upande wa maduka ya nguo za watoto ambapo anavishwa bure kwa mwaka mzima.

About Author

Advertisement

 
Top