Na.Ahmad Mmow.
Wapendwa, tunakutana tena, poleni kwa kutonisoma kwa siku kadhaa. Nisameheni sana, nimajukumu yamenikamata. Sijageuka nakuwa mmvivu asilani, bali kila siku majukumu yanaongezeka. Hongereni mliokwenye funga, kwani mlikotoka ni mbali kuliko mnakokwenda. Jipeni moyo, mtashinda.
Wapendwa, tunakutana tena, poleni kwa kutonisoma kwa siku kadhaa. Nisameheni sana, nimajukumu yamenikamata. Sijageuka nakuwa mmvivu asilani, bali kila siku majukumu yanaongezeka. Hongereni mliokwenye funga, kwani mlikotoka ni mbali kuliko mnakokwenda. Jipeni moyo, mtashinda.

Leo nitaanza andiko langu kwa kunukuu aya za kitabu kitatifu cha biblia. Nimedokoa katika kitabu cha agano la kale, maandiko ya nabii Suleiman(Solomon) yanayoitwa kitabu cha methali. Iwapo nitakuwa nimekosea jina la mwandishi niwieni radhi. Mjue tu, nitayatumia maneno hayo kwa nia njema. Kwani nakiheshimu na kukiamini sana sana kitabu hicho.
Lengo sio kukashifu dini na kitabu hicho. Bali nikutokana na hekima, busara na mafundisho yaliyomo ktk kitabu hicho ambayo ubora wake hauchuji wala kupauka hadi mwisho wa dunia, ndio unanifanya nitumie.
Imeandikwa; "njia yake huifadhi nafsi yake (ubinafsi, umimi, ulafi na tamaaa) tafsiri ni yangu" ambapo mtu wa aina hiyo hakosi kiburi kinachoweza kumsababishia anguko na maumivu makubwa. Thamani ya uzee huenda na busara na hekima kuu ambayo humtenga mtu na kiburi na ubinafsi. Kinyume cha hapo ni bure. Hata thamani ya mvi hutoweka na kubaki rangi tu, kama wapakazo vijana, ambao umri wao hausitahili kuwa na mvi.
Nimeanza na maelezo hayo ni katika kulinganisha yanayoendelea sasa katika kipindi hiki kuelekea kura za maoni kwa watangazania wa kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi. Tumeyasikia matamko ya wenye mvi na wasio na mvi. Hakika baadhi ya matamko yanaashiria kiburi cha wazi, tena baadhi ya wenye mvi wamewapa na mikono na kuwadhamini wenye kiburi. Hali iliyosababisha wenye mvi kutunishiana misuli kwa kiburi. Sisi wenye maarifa kidogo tumebaki kushangaa tusijue mwisho wa hayo.
Lakini katika kuonesha wamedhamiria kutunishiana
"Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu,kama kitaonekana katika njia haki (methali16:30) aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake (methali 17:18) njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu;yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.Kiburi hutangulia uangamivu;Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko,afadhali kuwa na roho ya ya unyenyekevu pamoja na umaskini, kuliko kugawanya mali pamoja na wenye kiburi (Methali,"( 16:17-19).
"Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu,kama kitaonekana katika njia haki (methali16:30) aliyepungukiwa na akili hupana mkono na mtu;na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake (methali 17:18) njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu;yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.Kiburi hutangulia uangamivu;Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko,afadhali kuwa na roho ya ya unyenyekevu pamoja na umaskini, kuliko kugawanya mali pamoja na wenye kiburi (Methali,"( 16:17-19).

Wapendwa tunaambiwa kwamba kichwa chenye mvi nitaji ya utukufu kama kitetenda katika njia za haki. Bila shaka umri mkubwa ndio wenye uwezo wa kukifanya kichwa cha mwenye umri kuwa na mvi. Ingawa wakati wa sasa mvi sio ishara ya uzee tena. Wanasayansi wanayo majibu ya kwanini hali hii. Umri mkubwa ndiyo msingi wa busara. Nabusara ndiyo husababisha mtu atende mambo kwa haki. Tena mwenye busara si hujitenga tu na uovu bali ukemea. Lakini daima ashikaye misuli wamechimbiana mikwala kwa matamko kama; huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono, na nguvu ya nyangumi akiwa majini tu. Mnapaonaa hapo jamani! uenda mafuriko tumeyaona na bila shaka tunayaona. Na hakuna aliyeweza kuyazuia. Kwa hali ilivyo natarajia kuona stunami itakayo sababisha vilio vitavyosababisha ukiwa na upweke kwa wenye kufiwa.
Naujua mchezo huu unaoitwa siasa unavyoweza kutengeneza washangiliaji na kuhamisha waombolezaji ghafla. Nguvu za nyangumi akiwa majini.Washangiliaji na waungaji mkono katika siasa huwa na matarajio mema kwa wanaye muunga mkono ili nao wanafaike. Lakini ikitokea waliyemuunga mkono ameanguka, inakuwa upweke na ukiwa kwa huyo aliye anguka.
Hiyo tisa, kumi ni wale wenye mvi tuliowategemea watakuwa na busara wametunishiana misuli. Kama sio kiburi tuite nini! Mwenye mvi mmoja anasema kujinadi mtangazania siyo kosa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama. Hivyo waliojinadi wapo sahihi.
Mwingine anasema mwenye haki ya kuwanadi ni chama nasiyo mtangazania mwenyewe. Mwisho wa mchezo huu nini! Maana haujaisha na unaendelea kupigwa. Ingawa sasa tupo katika kipindi cha lala salama. Bila shaka ni anguko kati ya pande hizo mbili. Ndipo tutakapo ishuhudia stunami itayosababisha vilio vya bandia, upweke na ukiwa. Mafuruko yame waacha watu salama ingawa wapo waliopoteza matumaini yakufikia malengo baada ya kukumbwa na mafuriko.
Lakini stunami hatapona muogeleaji, atakaye kuwa juu ya miti wala mapaa ya majumba. Sielewi stunami itatoka yalikotokea mafuriko au itaanzia yalikotokea mafuriko. Sijui! Lakini kulia kupo na huzuni ipo. Hayo hayana budi kutokea ili historia iweze kuandikwa vema. Shangiliaji na washangiliwaji jiandaeni kisaikolojia. Muda si mrefu yatajiri hayo, mwenye kubisha na asubiri kuona aweze kuamini. Wapendwa, siyo kila siku niwatafunie. Leo mjifunze kutafuna. Tuonane panapo majaaliwa.
Tags
MAKALA