MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga, Juni 27, mwaka huu wanatarajia kuvaana na SC Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kukusanya fedha za kujengea kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na walemavu wa ngozi, yaani albino.
Mapata yatakayo patikana moja kwa moja yatafanya shughuli kusudiwa kwa kuanza rasmi ujenzi wa kituo hicho huko Bagamoyo mjini Pwani.
“Tumeona klabu ya Yanga isipate sifa kwa kutwaa ubingwa tu, bali pia hata kufanya shughuli za kijamii kama hizi. Uongozi umebariki na hata Kocha Mkuu na benchi lote la ufundi lina taarifa na ndio maana tumeanza mazoezi mapema zaidi,tutashusha kikosi chetu cha kwanza chenye wachezaji wapya na wa zamani” alisema katibu mkuu Jonas Tiboroha.

Tags
SPORTS NEWS