Wanawake katika kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uch* kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka 10.

Wakati wa maandamano hayo, mawaziri wa serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.
Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakaazi wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi, mwanamke anapovua nguo na kusalia uch* ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake.

Chanzo : BBC Swahili
Tags
HABARI KIMATAIFA