Na.Ahmad Mmow.
Hamjambo wapendwa wa Tanzania wenzangu? Nianze kuwatakia kwa kuwaombea wale waliohawajiwezi walio hospitalini na majumbani wakisumbuliwa na maumivu ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali. Mungu awaponye haraka. Poleni na jamaa za wagonjwa ambao hakika nanyi mpo katika wakati mgumu kutokana na kuwauguza wapendwa wetu. Msikate tamaa mlionalo kubwa kwenu, kwa Mungu ni dogo. Kuweni wavulivu na wenye subira. Mungu awajaze nguvu ujasiri wahudumieni vema wapendwa wetu. Mchango wangu ni dua na maombi. Wenzangu na mimi mnaohangaika huku na kule msijue hatima yenu ya maisha mkikabiliana na ugumu wa maisha kiasi cha kushindwa kujua mtakula nini. Msikate tamaa bali ongezeni juhudi. BWANA hajawasahau, zamu yenu itakuja. Bado kidogo nanyi mtafikiwa, maana yeye hanatabia ya kumsahau yeyote. Sisimizi na wadudu wengine wadogo ambao ni vigumu kuonekana. Hajawasahau. Sembuse ninyi? Mtapata tu. Hakika wakuombewa ni wengi orodha ni ndefu. Bali yeyote popote alipo ambaye hana amani na furaha kutokana na sababu moja ama nyingine,namuombea pia. Hata hivyo niwaombe ninyi wote muungane nami kuliombea amani taifa letu ili amani iliyopo iendelee kuwa imara.
Hamjambo wapendwa wa Tanzania wenzangu? Nianze kuwatakia kwa kuwaombea wale waliohawajiwezi walio hospitalini na majumbani wakisumbuliwa na maumivu ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali. Mungu awaponye haraka. Poleni na jamaa za wagonjwa ambao hakika nanyi mpo katika wakati mgumu kutokana na kuwauguza wapendwa wetu. Msikate tamaa mlionalo kubwa kwenu, kwa Mungu ni dogo. Kuweni wavulivu na wenye subira. Mungu awajaze nguvu ujasiri wahudumieni vema wapendwa wetu. Mchango wangu ni dua na maombi. Wenzangu na mimi mnaohangaika huku na kule msijue hatima yenu ya maisha mkikabiliana na ugumu wa maisha kiasi cha kushindwa kujua mtakula nini. Msikate tamaa bali ongezeni juhudi. BWANA hajawasahau, zamu yenu itakuja. Bado kidogo nanyi mtafikiwa, maana yeye hanatabia ya kumsahau yeyote. Sisimizi na wadudu wengine wadogo ambao ni vigumu kuonekana. Hajawasahau. Sembuse ninyi? Mtapata tu. Hakika wakuombewa ni wengi orodha ni ndefu. Bali yeyote popote alipo ambaye hana amani na furaha kutokana na sababu moja ama nyingine,namuombea pia. Hata hivyo niwaombe ninyi wote muungane nami kuliombea amani taifa letu ili amani iliyopo iendelee kuwa imara.

Pesa za mataifa mbalimbali duniani.
Wapendwa, naendelea kutoa mchango na kutimiza wajibu wangu kama raia mwenzenu mtiifu kwa taifa na nchi yetu. Lengo nikukumbushana na kujadiliana. Mimi nitajitahidi kuwaeleza yale ambayo kwa fikra zangu naamini yatakuwa na faida kwetu sote. Naamini nitakuwa natoa mchango kwa taifa langu. Nikiungana kwa dhati na wenzangu ambao wanaumiza vichwa vyao kuona ninamna gani watatimiza uzalendo wao kwa taifa. Wote tunajua kwamba mwaka huu ni wauchaguzi. Tunatengeneza hatima(mustakabali wetu) ya maisha yetu ya kipindi cha miaka mitano ijayo. Mustakabali wa wawalemavu, vikongwe, wajawazito, vijana, wanawake, wakulima na wafanyakazi, wavuvi na wakwezi.
Wasomi na ngumbaru, matajiri na maskini, waajiri na waajiriwa. Nadhani mtakuwa mmeona jinsi uchaguzi ulivyo na umuhimu mkubwa kwetu kwanamna unavyogusa maisha na hatma ya kila mmoja. Ndipo tunatakiwa kutuliza akili na kuitumia nafasi hii kwa umakini na uangalifu mkubwa. Thamani ya uchaguzi ni kubwa kuliko vyote unavyomiliki hapo ulipo. Matokeo ya uchaguzi wetu yakiwa ya ovyo, ujue hata unavyomiliki vitasambaratika. Furaha uliyonayo itaondoka, matarajio mema ya mipango yako ya muda mfupi na mrefu itavurugika.
Wapendwa, kila uchaguzi ni mgumu kuliko uchaguzi ulitangulia. Uchaguzi ujao unachangamoto nyingi ambazo tusipokuwa makini zinaweza kugeuka na kuwa matatizo ambayo yanaweza kusababisha kuvurugana na kutoa neema kwa wachache ambao leo hawaitakii mema nchi yetu. Wakivuja mate kwa uchu wa kupora maliasili zetu ambazo MUNGU ameamua kutuonesha. Changamoto ni nyingi sana. Ebu angalieni zoezi zima linavyo kwenda mwendo zigizaga (shagalabagala). Uandikishaji hauendi kama ilivyotarajiwa. Uchaguzi mwezi octoba, lakini hadi sasa ni mikoa mitano tu imekamilisha uandikishaji. Mnapaonaje hapo! pamoja na hali hiyo tume imeendelea kutupa matumaini kwamba uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa. Na iwe hivyo, kwani haipendezi kuongozwa na viongozi waliomaliza muda wao. Ingawa tume hiyohiyo ilitupa matumaini ya kufanyika kwa kura ya maoni ya katiba mpya tarehe 30 Aprili lakini mwisho wa siku kura ya maoni imeota mbawa. Sababu zilizotolewa mlizielewa nyinyi wenzangu mliojaaliwa akili na maarifa.
Mimi mwenye akili mbili kasoro robo sikuelewa chochote naona tumezinguliwa tu. Bali hatuhukumu kwa historia na kosa ni mwalimu.
Ebu tuendelee kuiamini. Ugumu mwingine wa uchaguzi wa mwaka huu unatokana na changamoto ya maliasili zinazoendelea kugunduliwa nchini mwetu. Ikiwamo ugunduzi wa gesi asilia, maliasili ambayo imekuwa ni kama pacha wa shetani. Mafuta na gesi ni kama rafiki wa ibilisi. Rafiki huyu wa ibilisi amejitokeza mzimamzima katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Ndugu zangu nifuatilieni kwa makini sana. Maana hapa ndipo penye kiini cha makala yangu ya leo. Zipo changamoto nyingine zinahusu vyama vya siasa. Sipati picha kama baadhi ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi vitakuwa imara na salama. Nikitazama mtifuano baina ya wanachama wa wa CCM wanaotaka kuwania urais, kwa namnana baadhi yao yalivyoipania nafasi hiyo kiasi cha kuitumbulia macho na kujiapiza lazima waipate. Sidhani kama watakuwa radhi majina yao kuondolewa na vikao vya chama hicho. Ni bora wangeitumbulia na kuikamia bila kutumia nguvu kubwa. Lakini mabilioni ya shilingi wanayotumia yananitisha. Kiasi cha kutoamini kama wakiondolewa watakuwa tayari kumuunga mkono atakayepitishwa na chama hicho. Huku makada wengine wakijiapiza kuhama iwapo makada fulani wata pitishwa. Salama na amani ndani ya chama hicho itatoka wapi! Wazee wao ambao wangepoza mambo wameingiwa na mdudu pia. Wamejiingiza kwenye makundi ya wagombea. Karibu wana CCM wote wanachukua fomu kugombea urais. Balaa tupu! Wakuchaguliwa na kuchagua hajulikani sasa. Maana hata washabiki wamengia kiwanjani wanataka kucheza. Nikatazama UKAWA, sidhani nao kama watavuka salama. Mtifuano wa kugawana majimbo na nani awanie urais ni mtihani mzito.
Namna gani wataweka mizani katika kugawana ruzuku ambayo imekaa kimtego kwa masharti yake ni jaribio la hatari kwa ushirika huo. Yaani huku wanachinjana, kule wanafyekana. Tuachane na hayo ya vyama, kwani kwangu vyama siyo ishu kabisa hata vikifa sina chakupoteza. Mimi sio kwa ajili ya vyama bali vyama vipo kwa ajili yangu. Kwahiyo mimi nawewe ni muhimu kuliko vyama vya siasa. Ingawa baadhi ya watu ima kwa kutojua au kwa makusudi wameamua kujifanya hamnazo kwakujiona wapo kwa ajili ya
ya vyama.
Tumeziona changamoto hizo chache miongoni mwa nyingi. Lakini kama nilivyotangulia kueleza, kwamba kiini cha makala yangu ni changamoto ya ugunduzi wa maliasili gesi na hata madini ya urani kuwa safari moja na uchaguzi wa mwaka huu. Jamani tuwe makini sana kuhusu jambo hili. Tuanzie kujihoji na kuhoji sababu za watu kugeuka ghafla na kuwa na uchu wa fisi kuitamani nafasi ya urais. Tuzishugulishe akili zetu tupate sababu zenye mashiko. Kulikoni fujo hii, na nguvu za fedha walizonazo zimebeba siri gani? Mwenzenu nimeanza kuingiwa na hofu kubwa. Wengine wanadiriki kusema mabilioni hayo wanasaidiwa na marafiki. Nimuhimu tuwajue hao marafiki ni akina nani na wanarekodi gani, wanaishi wapi na wanafanya nini.
Napata hofu kuwa marafiki hao ni wale wasio itakia mema nchi yetu kutokana na uchu wa maliasili zilizogunduliwa. Kama ndivyo kwanini wasipenyeze rupia kwa watu ambao shida yao nikuitwa marais wala kwa muda wa siku mbili. Kwa nini wasipoteuliwa, watu wanaowafadhili wasiwachochee kufanya vurugu ndani ya nchi ili amani ivurugike waweze kuchukua raslimali zetu wakati tunavurugana baada ya zoezi la kupora kupitia vibaraka wao kushindwa? Watanzania tumeanza kuwa na utamaduni wa ajabu sana. Niwashangiliaji wa hatari, washangaaji na wakimbiliaji wa matukio ya hatari na mashabiki wa watengeneza hatari.
Ni tabia ambazo zitasababisha wasiotutakia mema tutumike kujivuruga na kujisambaratisha ili kuhalalisha wizi na uporaji wa maliasili zetu. Tusituke mapema, tuwakatae na tuwazomee wale ambao tunauhakika wanatumika.Uwingi wa kuwashangilia ugeuke kuwazomea. Wala tusiwaonee aibu, tutaharibikiwa. Tuchukue hatua sasa.
Siwatishi, bali natoa angalizo. Pindi yakitokea hayo walau wachache muweze kukukumbuka kwamba wachache tulipoteza muda kuwaonya. Majuto mjukuu, ajizi ni nyumba ya njaa, kama hujui kufa nenda kaone makaburi.
Tutaendelea kukumbushana.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. 0757115973/0717924695.
MUNGU IBARIKI TANZANIA. 0757115973/0717924695.
Tags
MAKALA