Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Mbio za kuwania urais zimezidi kunoga na kushika kasi. Baada ya leo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama, Bernad Membe kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya ofisi ya CCM mkoa wa Lindi iliyopo katika manispaa ya Lindi. Membe aliwaambia wananchi hao kuwa yeye ingawa anaitamani nafasi hiyo ya juu ya nchi, baada ya kujitathimini nakujiona anaiweza. Lakini hanamagunia ya fedha zitakazotumika kuwagawia wananchi ili achaguliwe kwa nafasi hiyo.
Alisema katika utumishi wa muda mrefu hajaiona biashara yoyote ikulu. Alisema hana mpango wa kununua urais kwani haoni raha yoyote ya kuwa rais kwa kuununua.
Membe akionesha dhahiri kukerwa na tabia ya kununua madaraka alisema yeye ni muadilifu na uadilifu wake siyo wa bandia bandia, hivyo kama akichaguliwa kuwa rais hatakuwa na huruma na watoarushwa. Ambao alisema wachache sawa na mafisadi. Akionesha kurusha kijembe kwa wenzake ambao wanatangaza kusaidiwa fedha na marafiki. Membe alisema tabia ya mafisadi na wala rushwa ni uongo kwani wanapotumia fedha za kifisadi wanasema wamesaidiwa na marafiki.
Membe akionesha dhahiri kukerwa na tabia ya kununua madaraka alisema yeye ni muadilifu na uadilifu wake siyo wa bandia bandia, hivyo kama akichaguliwa kuwa rais hatakuwa na huruma na watoarushwa. Ambao alisema wachache sawa na mafisadi. Akionesha kurusha kijembe kwa wenzake ambao wanatangaza kusaidiwa fedha na marafiki. Membe alisema tabia ya mafisadi na wala rushwa ni uongo kwani wanapotumia fedha za kifisadi wanasema wamesaidiwa na marafiki.
Hata kwenye mikutano yao kukiwa na wasikilizaji wacheche wanasema wapata watu wengi. Kuhusu uzoefu wake katika Chama Cha Mapinduzi: Alisema alijunga na chama hicho akiwa na miaka 22 tu, hivyo anakijua vema chama hicho kwani amelelewa na kukulia ndani yachama hicho. Ambapo pia alisema anauzoefu na amekidhi vigezo 13 vilivyoainisha na chama hicho kama sifa anazopaswa kuwa nazo mwanachama anayetakuwa rais kupitia chama hicho. Aidha kuhusu uzoefu serikalini, Membe alisema anauzoefu wa kutosha kwani ameanza kuwa serikalini tangu mwaka 1978 katika idara ya usalama wa taifa nakushika nyazifa mbalimbali ngazi ya kitaifa na kimataifa. Membe ambaye alitahadhirisha kuwa nafasi hiyo ni mzito nasiyo ya kufanyia mzaa na masihara kwani inahusu usalama wa nchi na wanachi wake hivyo siyo ya kuamka na kurupuka na kuitaka.Alisema alifanya tathimini na kujilinganisha na wenzake akabaini kuwa anawashinda.
Huku akibainisha wazi kuwa angemuona mtu anayemzidi vigezo na uwezo asingeomba. Nini vipaumbele vyake pindi akichaguliwa na kuwa rais:-
Sekta ya afya: Membe ambaye kwenye hutuba yake aliwasifu marais waliotangulia na rais wa sasa kwa utendaji mzuri, alisema atahakikisha anaimarisha huduma za afya kwa kuongeza idadi ya zahanati na hospitali na madawa ili wananchi wapate tiba zenye uhakika kwa kuwasogezea wananchi mahali walipo.
Uchumi:Alisema akichaguliwa atahakikisha nchi inakuwa kiuchumi kupitia kilimo, kwa kufufua na kuongeza viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuepuka kuuza mazao ghafi. Akiwahakikishia wananchi kuwa hilo linawezekana kwani tayari nchi inayo gesi asilia ambayo itatumika kuendesha viwanda hivyo. Kwani gesi iliyopo sikwa ajili ya matumizi ya majumbani pekee, bali ibadilishe uchumi kupitia viwanda. Alisema viwanda hivyo pia vitatengeneza ajira kwa wananchi hasa vijana.
Elimu: Membe aliyeanza hali ya kuwakosoa wale wanaoibeza serikali, ambao wanabeza juhudi za serikali na kuifanya kuwa agenda yao. Alisema hakuna awamu ambayo imejitahidi katika sekta hiyo kama awamu ya nne. Hivyo watu hao wasipokonye na kubeza kazi nzuri iliyofanywa na awamu hii katika sekta hiyo. Ambapo yeye alisema akichaguliwa atahakikisha kila wilaya inakuwa na chuo cha ufundi stadi ili vijana waliomaliza elimu ya msingi, sekondari na wakasome kwenye vyuo hivyo waweze kujia ajiri.
Ulinzi na usalama: Alisema suala la ulinzi na usalama atalipa uzito mkubwa kwa kuimarisha vyombo vya usalama ikiwamo jeshi la polisi kwa kuvipa vifaa vya kisasa na kiusalama ambavyo vitawekwa kila kona ya nchi. Alisema amesomea ulinzi na usalama hivyo hana mashaka kuhusu ulinzi na usalama wa nchi. Akibainisha kwamba dunia inakabiliwa na kitisho cha ugaidi. Nikatika eneo hili la ulinzi, Membe alitoa ujumbe mzito kwa waingizaji wa madawa ya kulevya na wauwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi(maalbino) wajiandae kushugulikiwa akiwa rais kwani hata kuwa na "salie mtume" hatakuwa na kigugumizi kuwashugulikia.
Sekta Binafsi.Alisema niwajibu wa serikali atayoiunda kushirikiana na sekta binafsi katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi. Hivyo serikali itashirikiana bega kwa bega na sekta binafsi ikiwamo kuanzisha benki itayotoa mikopo ili wenye biashara waweze kukopa na kupata mitaji. Nakubainisha kuwa hakuna nchi inayoweza kuendelea kwa kutegemea serikali bila kushirikiana na sekta binafsi.
Michezo: Membe kwenye hotuba yake hakuacha kuizungumzia. Ambapo alisema kama atachaguliwa atahakikisha nchi inaondokana na sifa ya kuwa kichwa cha mwendawazimu. Katika kuhakikisha hatuendelei kuonekana hivyo, serikali itaanzisha vyuo vya michezo na kuvipatia ruzuku ilikuviwezesha kujiendesha kwani michezo ni ajira. Pia alihaidi kupambana na wezi wa kazi za wasanii ili kukomesha wizi na dhuluma wanazofanyiwa wasanii kwa kuandaa mazingira mazuri ili wasiibiwe.
Utawala bora: Alisema ilikuweza kuwa na utawala bora lazima kiongozi awe muadilifu, ambao yeye anao uadilifu. Hivyo hatakuwa na kigugumizi na mafisadi na wala rushwa. Ambao alisema niwachache ingawa wanaonekana kama wengi kutokana na nguvu walizonazo. Huku akihaidi chama kitarejesha miiko ya uongozi ili kurahisisha kazi hiyo.
Akitoa wito kwa waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika vita ya rushwa na ufisadi kwa kufichua vitendo hivyo. Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar: Alihaidi kuulinda muungano uliopo ambao ni wakipekee na imara katika Afrika. Sanjari na kuyalinda mapinduzi ya Zanzibar, huku akihaidi kutokuwa na simile kwa mtu yeyote atayejaribu kubomoa muungano na kubeza mapinduzi. Awali aliyepata kuwa waziri na balozi, mzee George Kahama alimtaja Membe kuwa ndiye anayefaa kuwa rais kwani anasifa zote zinazohitajika katika nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi. Ikiwamo uzoefu, uadilifu, busara na kiwango cha elimu alichonacho.
Naye mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa alibeza kauli ya safari ya matumaini. Kwa kusema safari mzuri ni yamafanikio kwani kuishi kwa matumaini kunategemea vidonge (dawa) ambapo viikiisha nilazima mgonjwa atakufa.