LINDI NA MTWARA WASHAURIWA KUHUSU KUNUFAIKA NA GESI

Mwantum Mahiza
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantum Mahiza akitoa hutuba ya kufunga Mkutano wa wanajamii kuhusiana na Uundwaji wa mkakati wa mawasiliano wa kitaifa wa sekta ya Mafuta na Gesi Nchini, Mkutano ambao umewakusanya wadau mbalimbali wa mikoa ya Lindi na Mtwara, Mkutano huo ulifanyika Mkoani Mtwara hapo jana. 
(Picha na Fungwa Kilozo)
Mukhsin Rafi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi Ndg Mukhsin Rafi akichangia mada katika Mkutano wa wanajamii kuhusiana na Uundwaji wa mkakati wa mawasiliano wa kitaifa wa sekta ya Mafuta na Gesi Nchini, Mkutano ambao umewakusanya wadau mbalimbali wa mikoa ya Lindi na Mtwara, Mkutano huo ulifanyika Mkoani Mtwara hapo jana. 
(Picha na Fungwa Kilozo)
Mohamed Kem Kem
Mtangazaji wa Radio Pride Kutoka Mtwara Ndg Mohamed Kem Kem akichangia mada katika Mkutano wa wanajamii kuhusiana na Uundwaji wa mkakati wa mawasiliano wa kitaifa wa sekta ya Mafuta na Gesi Nchini, Mkutano ambao umewakusanya wadau mbalimbali wa mikoa ya Lindi na Mtwara, Mkutano huo ulifanyika Mkoani Mtwara hapo jana. 
(Picha na Fungwa Kilozo)

Na.Abdulaziz Ahmeid, Mtwara. 
Wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wameshauriwa wasifungwe na historia bali washiriki na kuzitambua fursa zitokanazo na gesi asilia iliyogunduliwa katika mikoa hiyo ili waweze kunufaika. Ushauri huo umetolewa Jana mjini Mtwara, na mgeni rasimi katika majadiliano juu ya matarajio makubwa na utengenezaji wa mkakati wa mawasiliano wa kitaifa wa sekta ya mafuta na gesi, ambaye ni mkuu wa mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza. Kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa majadiliano yaliyowashirikisha viongozi wa vyama siasa, viongozi vyama vya siasa, dini, wavuvi, wakulima, wafanyabiashara na waandishi wa habari.
Mkuu huyo wa mkoa alisema wananchi wa mikoa hiyo hawana sababu ya kupoteza muda kujadili mambo na matukio yaliyopita. Badala yake wajadili matarajio na mafanikio watakayopata na watanufaikaje na fursa zitokanazo na gesi asilia iliyogunduliwa katika mikoa hiyo.
Alibainisha kwamba siyojambo baya wananchi kuieleza na kuishauri serikali ifanye nini ili kuwa na muhafaka mzuri wenye tija katika sekta ya gesi na mafuta. Hatahivyo
isiwafunge na kupoteza muda kujadili, ingawa ni vigumu kuifuta.
Alisema sio rahisi wananchi wote kuajiriwa kwenye viwanda vitakavyojengwa katika mikoa hiyo. Hata hivyo kunafursa nyingine nyingi zinazoweza kuwafanya washiriki, wajiajiri na kunufaika na maliasili hiyo. Aliongeza kusema lengo la majadiliano hayo nikuimarisha mawasiliano baina ya wananchi na serikali katika sekta ya mafuta na gesi. Ili wananchi waweze kuwa na taarifa kwa uwazi kuhusiana na sekta hiyo ikiwamo kujua mapato yaliyopatika na mgawanyo wake.
Naye afisa uhusiano wa wizara ya madini na nishati, Badra Masoud, alisema serikali ipo katika hatua ya mwisho ya kutengeneza sera ya gesi. Hata hivyo imeona kuwa siyojambo jema sera hiyo kupitishwa bila kuijua. "Bila mkakati sahihi wa mawasiliano baina ya wananchi na serikali ni vigumu sera na hatasheria kueleweka" mkakati huu ni kwa ajili ya kukusanya maoni, kujenga mpango mpya wa baina wananchi wa Mtwara na Lindi", alisema Badra.
Mhandisi wa gesi wa wizara ya madini na nishati, Godfrey Mchele alisema sekta hiyo itakuwa na tija na kuwatoa walipo kuelekea maendeleo wataendelea kuwa na umoja na mshikamano, ambapo alibainisha kuwa sekta hiyo itakuwa ni kichocheo cha ukuaji wa sekta nyingine. 
Ibrahimu Mandowa, mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mtwara alisema ingawa mawasiliano na uwazi ni msingi wa amani kwa taifa, hata hivyo ni mambo madogomadogo tu yanayowekwa wazi. Lakini mambo makubwa hayawekwi wazi, ikiwamo mikataba ya madini.
Alhaji Mbulu alitaka maeneo ambayo yanagunduliwa maliasili lazima yaonekane mabadiliko ya maendeleo hasa katika huduma za jamii. Kwani pamoja na maeneo hayo kugunduliwa gesi lakini hakuna mabadiliko makubwa ya huduma za jamii.
Previous Post Next Post