
Basi la Another G kutoka Njombe kwenda Iringa limepata ajali usiku huu eneo la Kinyanambo Mjini Mafinga baada ya kugongwa na Lori inadaiwa watu 25 wamepoteza Maisha

****UPDATES YA AJALI***
WATU zaidi ya 10 wamepoteza maisha usiku huu katika ajali ya gari aina ya costa mali ya Another G inayofanya safari zake kati ya Njombe - Iringa baada ya kugongana na Lori.Taarifa za awali ambazo mtandao wa www.matukiodaima.co.tz umezipata kutoka eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Kinyanambo nje kidogo na mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wakati gari hiyo ya Another G ikitokea Njombe kwenda Iringa
Mbali ya kuwa maiti ambazo zimetolewa na kufikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya wilaya ya Mufindi kuwa zimekwisha fika zaidi ya 25 ila inadai kuwa idadi ya miili inaweza kuongezeka zaidi kutokana na kazi ya uokoaji ikiendelea eneo la tukio.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita ameuthibitishia mtandao huu wa matukiodaima kwa njia ya simu juu ya ajali hiyo na kueleza kuwa ni miongoni mwa ajali mbaya kutokea wilayani Mufindi .
Tags
HABARI ZA KITAIFA