Klabu za AS Monaco na Lazio huenda zikapambanishwa na mashteni wekundu Man Utd, katika mchezo wa hatua ya mtoano wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2015-16.

Man Utd wataanzia katika hatua ya mtoano baada ya kumaliza kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya nchini England msimu wa 2014-15 na klabu hizo za nchini Ufaransa pamoja na Italia zinatajwa kuwa miongoni mwa wapinzani wa mashetani wekundu.
Shiriksiho la soka barani Ulaya UEFA tayari limeshatoa ratiba ya michezo ya hatua ya mtoano hatua ya awali ambapo timu kumi nguli kutoka mataifa tofauti ya barani humo zitaanza kupambana Julai 28/29 na kisha August 4/5 kabla ya kwenda katika hatua ya mwisho ambayo itawapata watakaoingia kwenye mchakato wa makundi.
Hata hivyo nani atapambana na nani bado haijafahamika kwa undani lakini taarifa za awali zinaeleza huenda Man utd wakapata mtihani wa kupambanishwa na mmoja kati ya vigogo hivyo viwili.
Ikumbukwe kwamba Man Utd hawakushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2014-15, kutokana na kukosa sifa ya kucheza michuano hiyo baada ya kumaliza kwenye nafasi ya saba katika msimamo wa ligi ya nchini England msimu wa 2013-14.

Tags
SPORTS NEWS