
Usiku wa Kuamkia leo watanzania walishuhudia Tuzo za Kilimanjaro zilizotolewa katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo wasanii Kibao walikuwa miongoni mwa washiriki katika tuzo hizo katika Vipengele Tofauti. Lakini kivutio kikubwa kilikuwa katika wasanii wawili ambao wenye Ushindani mkubwa kwa mashabiki wao ambao ni Alli Kiba na Diamond Platnumz ambapo masikio ya wengi yalikuwa yakitega kusikia nani anaondoka na Tuzo Nyingi kumzidi mwenzake.
Hakika Diamond aliweza kuweka Rekodi nzuri mwaka 2013-2014 kwa kunyakua Jumla ya Tuzo saba katika Tuzo hizo za KTMA, Kwa mwaka Huu 2014-2015 aliyeongoza katika Tuzo hizo ni Ali Kiba kwa kuweza kunyakua Tuzo 5 huku Diamond Platnumz akiachwa mbali kwa kunyakua Tuzo 2 pekee,
Hivyo kwa matokeo hayo Bado Rekodi ya Diamond ya Msimu wa 2013-2014 kushindwa kuvunjwa na Msanii wowote yule.
Na hii Hapa ni Orodha Kamili ya Tuzo za Washindi Katika Vipengele Tofauti:
TUZO YA HESHIMA (ALLOFFAME) - CAPT. JOHN KOMBA (R.I.P)

KIKUNDI BORA CHA MWAKA - BONGO FLEVA - YAMOTO BAND
KIKUNDI BORA CHA MWAKA TAARAB - JAHAZI MODERN TAARAB
MSANII BORA CHIPUKIZI - BARAKA DA PRINCE
WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA (WAITE) -MRISHO MPOTO FT. FELLY KANO

WIMBO BORA WA AFRO POP - MWANA ALI KIBA
MTUNZI BORA WA MWAKA BONGO FLEVA - ALI KIBA
MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIUME - ALI KIBA
MWIMBAJI BORA WA KIUME BONGO FLEVA - ALI KIBA
WIMBO BORA WA MWAKA (MWANA)- ALI KIBA

WIMBO BORA WA MWAKA WA KUSHIRIKISHWA - (KIBOKO YANGU) MWANA FA & ALI KIBA
VIDEO BORA YA MWANAMUZIKI YA MWAKA - MDOGOMDOGO - DIAMOND PLATINUMZ
WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA - NITAMPATA WAPI - DIAMOND PLATINUMZ
BENDI BORA YA MWAKA - FM ACADEMIA
MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA BENDI - EMOROSO
MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA TAARABU -ENRICO
WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI (WALEWALE) -VIJANA WA NGWASUMA

MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA BONGO FLEVA - NAHREEL

MTUNZI BORA WA MWAKA- HIP HOP - JOH MAKINI
MSANII BORA WA HIP HOP - JOH MAKINI
MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - JOSE MARA

MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIKE - VENESSA MDEE
MWIMBAJI BORA WA KIKE BONGO FLEVA - VANESSA MDEE
MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - MZEE YUSSUF
MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB- MZEE YUSSUF
MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB - ISHA MASHAUZI
WIMBO BORA WA TAARAB (MAPENZI HAYANA DHAMANA)- ISHA MASHAUZI

WIMBO BORA WA R&B (SIKSIKII)- JUX
RAPA BORA WA HIP HOP - KIPI SIJASIKIA ( PROF J FT. DIAMOND PLATINUMZ)
WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI (SURA YAKO) - SAUTI SOL
Tags
HABARI ZA WASANII