Baadhi ya viongozi wa vya siasa vya upinzani, wilayani Liwale mkoani Lindi. Wameunga mkono mbio za mwenge wa uhuru na kuwabeza wanaopinga uwepo wa mwenge wa uhuru.Wakizungumza na waandishi wa habari waliokatika msafara wa mbio za mwenge mjini Liwale hapo juzi.Viongozi hao wa vyama vya CHAUSTA,CHADEMA,NCCR-MAGEUZI na CHAUMA.Walisema mwenge wa uhuru ni alama na nembo bora ya taifa,na unawaunganisha watu wa itikadi tofauti za siasa,dini,rangi na makabila.Nakuwafanya wajione ni wamoja.
Kamishna WA NCCR-MAGEUZI mkoa wa Lindi, Zuberi Kandile. Alisema Mwenge unawaunganisha wa Tanzania, nakusababisha wajione ni wamoja bila kujali tofauti zao za itikadi za siasa, dini, rangi wala kabila. Alisema licha ya kuwaunganisha na kuwafanya wawe wamoja, lakini pia mwenge unapofungua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo wanapata fursa ya kujifunza na kuthibitisha utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kama kilivyowaahidi wananchi.
"Pia kwakuwa serikali ya wilaya inatushirikisha katika hatua zote,tunapata nafasi ya kujua na kulinganisha thamani ya fedha zinazotumika na miradi inayotekelezwa".
"Vilevile ujumbe wa mbio za mwenge unafaida kwetu, sasa tunatekeleza ilani ya chama tawala, kama kunasababu za kuuweka katika jumba la makumbusho ni hapo tutakaposhinda nasiyokupinga wakati hatuja unda dola tutakuwa hatueleweki," alisema Kandile.
Mwenyekiti wa wilaya hiyo,wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) Athuman Mohamed.Licha ya kuungana na wenzake kusema mwenge unafaida lakini pia aliusifu na kuishukuru serikali ya wilaya hiyo kwa kuvipa ushirikiano vyama hivyo katika matukio yote ya kiserikali.
Alisema wamesukumwa kushiriki kikamilifu mbio hizo kwakuwa serikali inawatambua na kuwathamini." mkuu wa wilaya unasaidia kuisukuma serikali itekeleze miradi mbalimbali ya maendeleo.Nakutoa wito kwa wanaoubeza na kuupinga,waache kufanya hivyo.Kwani licha ya kuisukuma serikali itekeleze ujenzi na kazi za maendeleo,lakini mwenge ni alama ya kuwaenzi waasisi wa taifa hili."kuuweka jumba la makumbusho ni kuenzi,lakini kuukimbiza nizaidi ya kuuenzi.Maana unahubiri upendo na unawafanya wananchi ambao hawaijui historia ya nchi waweze kuijua".
Mkuu wa wilaya ya Liwale,Ephraim Mmbaga alikiri kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vilivyo katika wilaya hiyo kwenye matukio ya kiserikali kwakuwa vyama hivyo ni wadau wakubwa wamaendeleo iwapo vitashirikishwa na kuthaminiwa.