Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Wananchi mkoani Lindi, wametakiwa kutunza miradi ya maendeleo iliyojengwa katika maeneo yao ili iweze kudumu na kuwasaidia kwa kipindi kirefu.Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti mkoani Lindi, na kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka huu, Juma Khatib Chum katika wilaya na halmashari zilizopo mkoani Lindi, wakati Mwenge ulipokimbizwa katika mkoa huu.
Juma alisema wananchi wanawajibu wa kuitunza miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kujengwa na iliyojengwa kwenye maeneo yao kwani uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya wananchi na hata viongozi wa umma hawaithamini na kuitunza iliyopo kwenye maeneo wanayoishi na wanayofanyia kazi.
Alibainisha kuwa uzalendo nipamoja na kuthamini na kuitunza miradi ya maendeleo ambayo inapokuwa imekamilika na kukabidhiwa jamii au taasisi inakuwa ni mali ya umma.
"Miradi inayowekwa mawe ya msingi,inayofunguliwa na kuzinduliwa ni lazima itunzwe iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu tunataraji miradi yote itatunzwa vizuri ili miradi mipya mingine iweze kujengwa," alisisitiza Juma.
"Miradi inayowekwa mawe ya msingi,inayofunguliwa na kuzinduliwa ni lazima itunzwe iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu tunataraji miradi yote itatunzwa vizuri ili miradi mipya mingine iweze kujengwa," alisisitiza Juma.
Juma aliongeza kusema serikali inajitahidi kujenga na kuchangia miradi ya maendeleo inayoibuliwa na wanachi wenyewe.Hata hivyo baadhi ya wananchi wanakwamisha juhudi hizo kwa kuhujumu na kuiharibu. Alitaja baadhi ya miradi inayohujumiwa mara kwa mara ni miundombinu ya barabara,maji na umeme.
Sanjari na wito huo, Kiongozi huyo aliwatahadharisha na kuwaomba wananchi wa mkoa huu kuwakataa na kutowachagua watu wanaotoa rushwa ili wachaguliWe na kuwa viongozi. Alisema watu wanaotoa rushwa wanadhihirisha kuwa hawana uwezo wa kuongoza, na iwapo watachaguliwa watakuwa ni viongozi wabovu.
"Ndugu zangu.mtu unaweza kuoa mwanamke mbovu au kuolewa na mwanaume mbovu lakini siyo kuchagua kiongozi mbovu, sababu ndoa mnaweza kutengana wakati wowote" lakini kiongozi mbovu ataendelea na ubovu wake hadi ufike uchaguzi mwingine ndipo mtapata fursa ya kuachana nae,"alionya Juma.
Katika hatua nyingine, miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 2,043,117,556.00, imefunguliwa,kuzinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi,na mwenge wa Uhuru wilayani Kilwa.Hayo yamesemwa jana Kilwa masoko, na mkuu wa wilaya hiyo, Abdallah Ulega,alipokuwa anasoma risala ya utii kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Mbele ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa.