Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii (TASAF) imetumia shilingi 301.94 milioni, kwa ajili ya kuvijengea uwezo vikundi vya vijana vya uzalishaji mali 21.
Hayo yameelezwa leo mjini Liwale, na mkuu wa wilaya ya hiyo, Ephraim Mmbaga alipokuwa anasoma risala ya utii kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015, Juma Khatib Chum.
Mmbaga alisema ilikutekeleza nia njema ya serikali ya kuwapatia mitaji vijana ili waweze kujiajiri kupitia vikundi vya uzalishaji mali.
Wilaya hiyo kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii imevisaidia vikundi 21 vyenye wanachama 381, vikiwemo: vikundi 8 vya ushonaji, vikundi 2 vya ubanguaji korosho na vikundi 8 vya kilimo cha bustani za umwagili kwa njia ya matone.
Alisema wilaya hiyo inatambua dhamira njema ya serikali ya kuwapelekea maendeleo wananchi, hivyo makundi ya kijamii yanastahili kupewa stadi za maisha, hususani ujasirilia mali. "Hadi sasa wilaya hii inavyama ushirika vya kuweka na kukopa 12 vikundi vya wanawake vya ujasiriamali 36 na vikundi vya VICOBA 26,"alisema Mmbaga.
Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kusema wilaya hiyo inavikundi vya hisa 140 vyenye wanachama 3183 ambavyo akiba za michango ya wanachama yenye jumla ya shilingi 200,989,296.00 ambavyo vimeanzishwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kupitia mradi wa Mwanamke Mwezeshe.
Hatua ambayo imerahisisha upatikanaji wa mitaji yenye masharti nafuu. "wilaya itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuyawezesha makundi haya,kutoa elimu ya ujasiriamali na kuhamasisha makundi haya yajiunge na SACCOS au VICOBA," alisema.
Kuhusu maandali ya uchaguzi mkuu ujao, Mbaga alisema wilaya hiyo imejipanga vizuri kwani wananchi wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha. Ambapo hadi sasa Wilaya hiyo yenye watu 91,380 imefanikiwa kuandisha watu 26,698 kwenye daftara la wapiga kura. Ambayo ni sawa na asilimia 51.21 ya lengo la kuwa andikisha watu 51,698.
Jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi 2.14 bilioni ilitembelewa, kuzinduliwa, kufunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi katika wilaya hiyo. Ambapo wananchi wamechangia shilingi 553,793,484.00, wahisani shilingi 1,007,020,981.63, halmashauri ya wilaya ya Liwale, shilingi 56,880,000.00 na serikali kuu shilingi 55379384.00.