TFDA YATEKETEZA VIDOZI,VYAKULA NA MADAWA YASIYOFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU.

Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Mamlaka ya chakula na madawa nchini (TFDA) jana ilichoma moto vyakula, vinywaji na vipodozi visivyositahili kwa matumizi ya kibinadamu.
taswira ya Lindi
Taswira Maridhawa Kutoka Katikati ya Mji wa Lindi

Zoezi hilo ambalo utekelezaji wake ulisimamiwa na maafisa wa afya wamkoa wa Lindi, halmashauri ya manispaa ya Lindi na mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kusini lilifanyika katika manispaa ya Lindi. Ambapo vipodozi, vinywaji na vyakula vyenye thamani ya shilingi 19.26 milioni, ambavyo muda wake wa matumizi ulikuwa umekwisha, viliteketezwa kwa kuchomwa moto.

Akizungumza na waandishi wa habari walikwenda kushuhudia tukio la uteketezaji huo, kaimu meneja wa mamlaka ya chakula na madawa wa kanda ya kusini, Juma Bukuku. Alisema uteketezaji huo umetokana na msako uliofanyika katika halmashauri ya manispaa na wilaya ya Lindi uliofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu kwenye maduka mbalimbali yaliyo kwenye halmashauri hizo.

Alisema baadhi ya bidhaa zilichomwa moto zilikwisha muda wake wa matumizi, zisizo sajiliwa na zilizokatazwa kutumiwa hapa nchini kutokana na kuwa na madhara kwa watumiaji.
"kunavipodozi ambavyo vilikatazwa kutumika tumevikuta madukani, baadhi ya bidhaa hazina usajili na hata lugha iliyoandikwa haileweki na bidhaa nyingine zimekwisha muda wake wa matumizi, lakini tumevikuta madukani vinauzwa, jambo ambalo halikubaliki". 

Kaimu meneja huyo alibaisha kuwa wafanyabiashara wengi hawatunzi kumbukumbu muhimu zinazoonesha walinunua wapi. Hivyo kusababisha ugumu wa kujua ni nani wanaingiza bidhaa zilizopigwa marufuku kutumika. Alisema misako itakuwa endelevu, nakuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo na maafisa wa idara ya afya waliokaribu katika maeneo wanayoishi. 

Pia meneja huyo aliwaasa wananchi kusoma maelezo yaliyo kwenye vifungashio vya bidhaa wanazonunua ili waweze kujua kama bidhaa hizo zinaviwango vyenye ubora unaokubalika kisheria. Ikiwamo kujua muda wa matumizi, mahali zilikotengenezwa, na kama zimesajiliwa.

Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na vipodozi vyenye thamani ya shilingi 16,181,540.00, Madawa yenye thamani ya shilingi 939,500.00 na vyakula vyenye thamani ya shilingi 2,143,400.00.
Previous Post Next Post