Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Kiasi cha shilingi 7.63 bilioni, zinatarajiwa kutumika kwa ujenzi wa miundo mbinu katika halmashauri ya manispaa ya Lindi.
Kampuni tatu ndizo zilizoteuliwa kufanya kazi hizo ni Namis Corporate Engineering and Contractors itakayo jenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 6.2 kwa gharama ya shilingi 6.230 bilioni.
Kiasi cha shilingi 7.63 bilioni, zinatarajiwa kutumika kwa ujenzi wa miundo mbinu katika halmashauri ya manispaa ya Lindi.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kelvin Makonda wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba, kati ya halmashauri hiyo na kampuni za ujenzi zilizoteuliwa kufanya kazi za ujenzi huo. Makonda alisema mchakato wa zabuni kwa ajili ya kuwapata wakandarasi watakaotekeleza kazi za ukarabati na ujenzi ulianza tarehe 7 mwezi Novemba mwaka jana, kwa kutangaza zabuni ya kuwapata wakandarasi wenye sifa pamoja na mtaalam kwa ajili ya usimamizi wa kazi husika.
"Aidha kwa upande wa mtaalam mshauri kampuni ya Advanced Engineering Solution Limited ya Dar esSalaam ndiyo iliyotunukiwa zabuni kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya miundombinu katika manispaa yetu"anapaswa kutekeleza kazi yake katika kipindi cha miezi 12 kuanzia mwezi wa juni mwaka huu kwa gharama ya shilingi 278.180.00 milioni,"alisema Makonda.
Mkurugenzi huyo aliitaja miradi hiyo kuwa ni ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 6.2, ujenzi wa machinjio ya kisasa na ujenzi wa ujenzi wa uzio wa kuhifadhi taka ngumu. Aliongeza kusema kwamba miradi hiyo ni mikubwa, hivyo itasababisha mabadiliko makubwa ya miundombinu iliyopo katika manispaa hiyo, nakuchochea harakati za kiuchumi.
Meya wa halmashauri hiyo, Frank Magali alisema ili miradi hiyo iweze kuwa na ubora, kunahitajika ushirikiano katika usimamizi wakati ujenzi wa miradi hiyo ili iwezekuwa namatokeo mazuri.
Naye mkuu mkuu wa wilaya ya Lindi, Yahya Nawanda alizitaka kampuni zilizoteuliwa kujenga miundombinu hiyo kuheshimu mikataba. Ikiwamo kumaliza kazi kwa wakati na ubora wa kazi watakazo fanya. "kukiwa na ubabaishaji hatusita kuwasimamisha, mikataba yote ipo wazi mambo ya variesheni (ongezeko) hatuhitaji," alisema Nawanda.
Kampuni tatu ndizo zilizoteuliwa kufanya kazi hizo ni Namis Corporate Engineering and Contractors itakayo jenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 6.2 kwa gharama ya shilingi 6.230 bilioni.
Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering corparation, itakayojenga machinjio ya kisasa kwa gharama ya shilingi 693.98 milioni na Madwala (T) Limited itakayojenga uzio wa kuhifadhia taka ngumu, kwa thamani ya shilingi 427.180 milioni.