NAY WA MITEGO ANOGEWA NA SHAMSA SASA ATANGAZA NDOA...!!

Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, ameeleza kuwa endapo staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford ambaye sasa hivi wanapika na kupakua, atamuonesha utulivu na uaminifu hataona sababu ya kutomuoa.
Shamsa Ford
Nay aliyasema hayo juzikati alipokuwa akizungumzia mipango yake na Shamsa ambaye amejiweka kwake baada ya kutosana na mzazi mwenzake, Siwema. Nay alisema:

“Hilo la ndoa kiukweli kabisa kama Shamsa ataonesha kutulia na kunithibitishia kuwa hatakuja kunizungua, sitaona hatari kumuoa.”

Source:: GPL
Previous Post Next Post