MSICHANA WA MIAKA 17, ABAKWA NA WANAUME 40

Je jamii yako imeathirika vipi na ukatili wa kijinsia?, Soma kisa cha kusikitisha cha Msichana mwenye chini ya umri wa miaka 18 aliyebakwa na wavulana zaidi ya 40,
Ubakaji
Katika moja ya makala gazeti la Sunday Times, Msichana mmoja jamii ya Yazidi, huko Syria ameweka wazi mateso aliyokuwa akipewa na kundi la wapiganaji wa kiislamu wa ISIS na kusema kwamba aliwahi kubakwa na wanaume wapatao 40 nakutolewa usichana wake.

Msichana huyo ambaye (jina limehifadhiwa) sasa ni mjamzito wa miezi 9, amesema kila siku alikuwa akibakwa na wanaume wapatao 40, na walikuwa wakifanya hivyo kwa zamuzamu na alipojaribu kukataa alimwagiwa maji ya moto.

“Kuna kipindi nilitakiwa nichague kati ya kifo na kulazimishwa kuafanya mapenzi, lakini vyote ilikuwa sawa na kifo hivyo niliwaambia wafanye wanachokitaka”, alisema msichana huyo.

Wasichana na wanawake wa Kiyazidi wanalazimishwa kufuata misingi ya dini ya kiislamu, na wakikataa wanakutana na adhabu kali ya kubakwa au kuuliwa, kitendo kinachowafanya wengi wakimbie nchini mwao.

Habari zinaeleza wapiganaji wa ISIS wameshaua wanawake na wasichana wengi jamii ya Yazidi, huku wengine wakiwakamata na kuwafanya watumwa kwenye kambi zao.

Nchi ya Syria imekumbwa na machafuko ya kisiasa kwa takribani tangu miaka mitano iliyopita ambapo baadi ya raia wanapinga uwepo wa madarakani kwa Rais wa nchi hiyo Bashar al-Assad , na machafuko hayo sasa yanapelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe huku udini ukianza kuchukua nafasi.
Previous Post Next Post