MABINGWA WA UJERUMANI WAJITOSA KUMUWANIA DI MARIA

Mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, wameripotiwa kuwa katika mazungumzo na uongozi wa klabu ya Man Utd yaliyolenga usajiliwa wa mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina Ángel Fabián Di María Hernández.
Ángel Fabián Di María Hernández.
Jarida la michezo la nchini Ujerumani liitwalo “Kicker” limefichua ukweli wa vikao vinavyoendelea baina ya viongozi wa pande hizo mbili lakini haikueleza ni wapi walipofikia katika mazungumzo yao.

Jarida hilo pia limefichua siri ya mabingwa hao wa nchini Ujerumani kuwa katika mipango ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji pamoja na klabu ya VFL Wolfsburg, Kevin de Bruyne.

Mkataba wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 wa kuitumikia klabu ya VFL Wolfsburg unatarajia kufikia kikomo mwaka 2019, hatua ambayo imeripotiwa huenda FC Bayern Munich wakamsajili De Bruyne kwa kiasi kikubwa cha pesa.

Mkurugenzi mtendaji wa FC Bayern Munich, Michael Reschke ndiye ameripotiwa kuwa mstari wa mbele katika harakati za usajili wa wachezaji hao wawili, na ameonyesha kuwa na matumaini makubwa ya kufanikisha azma iliyowekwa na uongozi wa klabu hiyo.

Di Maria ambaye alivunja rekodi ya usajili ndani ya klabu ya Man Utd kufuatia ada yake ya uhamisho kufikia paund million 59.7 akitokea Real Madrid ya nchini Hispania, amekua hana msimu mzuri tangu alipojiunga na mashetani wekundu mwanzoni mwa msimu wa 2014-15.

Njia sahihi ambayo imeainishwa na meneja wa klabu ya Man Utd, Louis Van Gaal ni kumuweka sokoni Di Maria kwa lengo la kuiwezesha klabu hiyo kurejesha pesa ambazo zitafanikisha usajili wa wachezaji wengine katika majira ya kiangazi.
Previous Post Next Post