Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID SADIKI MGENI RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA CHANJO TANZANIA, VIWANJA VYA ZAKHIEM MBAGALA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akiongea na wananchi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam ...
Maazimiso ya Chanjo
Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema akiongea na wananchi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam

Maazimiso ya Chanjo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Sadiki akiongea na wananchi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam ambapo aliwataka wananchi kujitokeza kwawingi kupata chanjo hiyo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema.

Maazimiso ya Chanjo

Wasanii wa kikundi cha Hamasa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa alipokuwa akiongea na mananchi walio jitokeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Zakhiem.

Maazimiso ya Chanjo
Mganga Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, mama Mugisha kulia.akiwaongoza Viongozi malimbali kwenda katika Banda maalumu lililo andaliwa kwa Mkuu wa Mkoa kuwapatia chanjo watoto waliofika katika maadhimisho hayo kupatiwa chanjo
Maazimiso ya Chanjo
Mtoto Mbahi Simon (Miezi 2), aliyepagatwa na mama yake Joyce Joseph(30), mkazi wa Charambe akipatiwa chanjo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Sadick katika maadhimisho ya wiki ya chanjo Tanzania, yaliyofanyika viwanja vya Mbagala Zakhiem Jijini Dar es Salaam.

Mjomba band
Mjomba Band ikitoa burudadani wakati Maadhimisho hayo
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


NA. SALHA MOHAMED, DAR ES SALAAM
KINGA ni bora kuliko tiba,”. Hii ni moja ya misemo ambayo watanzania wengi hupenda kuitumia pale ambapo kuna tahadhari au uhitaji wa jambo fulani kufanyika ili kuepusha janga fulani.Hali hiyo inakuja pale tu mtu huyo kushindwa kupata huduma za afya hadi anapozidiwa kwa ugonjwa fulani ndipo apate tiba kwa daktari. 

Chanjo ni silaha kali katika kinga na udhibiti wa magonjwa ya maambukizi, Kutumia chanjo kwa kinga na udhibiti wa magonjwa ya maambukizi kwa kutumia chanjo ni mafanikio makubwa waliyoyapata binadamu katika mapambano dhidi ya magonjwa ya maambukizi.

Naweza kusema kuwa chanjo ni dawa inayotengenezwa kwa kutumia vijidudu au virusi vinavyosababisha magonjwa ya maambukizi, na virusi hivyo vikiingia kwenye mwili wa binadamu, mwili huo utatoa kitu fulani ambacho kinaweza kuzuia virusi hivyo visiingie tena mwilini.
Watu wengi wamekuwa wakisema chanjo husababisha magonjwa mbalimbali, hiyo siyo kweli, chanjo haisababishi magonjwa katika mwili wa binadamu bali inaweza kulinda afya ya binadamu kutokana na maradhi mbalimbali kutokana na maradhi.

Kutokana na umuhimu wa chanjo katika kinga ya mwili na udhibiti wa magonjwa ya maambukizi, nchi mbalimbali duniani zinatilia maanani sana kazi ya kutoa chanjo.

Tanzania ni mojawapo ya nchi hizo ambapo hivi karibuni Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Said Sadick, ameadhimisha kilele cha wiki ya chanjo Tanzania ambayo huadhimisha Afrika nzima na lengo ni kuhamiasha jamii kutumia huduma za chanjo.

Hakika ni jambo la kujivunia kwani mikakati na juhudi zinazofanywa na Wizara kupitia mpango wa Taifa wa chanjo katika kupunguza magonjwa na vifo vya watoto vinavyozuilika kwa chanjo.

Sadick anasema Kiwango cha matumizi ya chanjo kwa watoto ni zaidi ya asilimia 100 kwa sababu watumishi wamekuwa wakichanja watoto hata nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema chanjo ni zawadi ya maisha, pia imethibitika kuwa chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza magonjwa na kupunguza vifo vya watoto na kupunguza gharama za matibabu.

“Takwimu za kitaalamu zimethibitisha kuwa chanjo huzuia takribani vifo milioni 2 hadi 3 kila mwaka vinavyotokana na maradhi yanayozuilika kwa chanjo duniani,

“Mtakumbuka 1990, tulishuhudia wodi za surua zikifungwa na vifo kupungua na pia kupooza kutokana na polio kutoweka, hivi leo, kuna watu hawajawahi kuona mgonjwa wa polio alivyo,” alisema

Anasema mafanikio hayo ni matokeo ya kuwekeza katika chanjo ambapo jumla ya watoto 1,682,015 kati ya 1,733,967 ambayo ni sawa na asilimia 97 ya watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja kwa 2014 walipata chanjo.

Anafafanua kuwa mafanikio hayo yametokana na serikali kufanikiwa kutoa chanjo kwa watoto walengwa kiasi cha kufikia asilimia 90 ya kiwango cha chanjo kinachokubalika kitaifa na kimataifa kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja.

Anaongeza kuwa bado kuna changamoto ya watoto ambao hawajapata au hawajakamilisha ratiba ya chanjo kulingana na umri wao, ambapo watoto hawa wapo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa na kuhatarisha afya ya jamii nzima.

“Magonjwa yanayolengwa na mpango wa Taifa wa chanjo kwa sasa ni Kifua kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Polio, Surua, Rubella, Pepopunda, Homa ya ini, Homa ya uti wa mgongo, Kichomi, Kuhara na Saratani ya mlango wa kizazi,” alisema Sadick

Ili kulinda vizuri afya ya binadamu, hivi sasa, wanasayansi na wataalam wa tiba zimepatikana chanjo mpya za kuzuia magonjwa ya shingo ya mlango wa kizazi na kuzuia ugonjwa wa polio ambapo zingine bado zipo katika hatua ya mbalimbali za majaribio zikiwemo za Ukimwi na Malaria.

Hatua hiyo ya serikali kwakushirikiana na wizara ya afya imejitahidi katika kuhakikisha chanjo za magonjwa hayo zinapatikana na kutolewa bila malipo kwa watoto wanaostahili chini ya miaka mitano.

Amezitaka halmashauri kuhakikisha kuwa wanapoandaa mipango, huduma za chanjo zipewe kipaumbele zikiwemo huduma za mkoba ili kumfikia kila mtoto, upatikanaji wa mitungi ya gesi kwenye vituo.

Uhamasishaji jamii kuhusu umuhimu wa huduma za chanjo, mafuta kwa ajili ya usambazaji wa chanjo, Usimamizi elekezi na mafunzo ya chanjo kwa watumishi wapya yanatolewa kwa wakati muafaka.

Pia, anaongeza kuwa wazazi walezi na familia kupeleka watoto wanaostahili kupata chanjo vituoni ili wakapate chanjo hizo stahiki kwa ratiba ili kujikinga na maradhi kama polio ambao ni hatari kwa watoto.

“Kila mmoja anawajibu anawajibu kuhakikisha mtoto wake, mtoto wa jirani au mototo yoyote yule anapewa haki ya kupata chanjo na asiwe hatari kwa wengine dhidi ya magonjwa ya mlipuko, ambapo walengwa ni watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano ambao hawajapata au hawajakamilisha ratiba ya chanjo kulingana na umri,”anasema.

“Napenda kuihakikishia jamii kuwa chanjo zote zinatolewa nchini ni salama na zimedhibitishwa na Shirika la Afya Duniani na nchi zote za dunia ikiwemo Tanzania,” anasema

Aidha mamlaka ya chakula na dawa imekuwa ikikagua chanjo zote zinazoingia nchini ili kuhakikisha kuwa chanjo zote zinazoingia ni zile tu zenye ubora na zimepitiwa na Shirika la Afya Duniani.

Kwahali hiyo jamii inapaswa kujua umuhimu wa kupeleka watoto wao kupata chanjo kwani tayari serikali imetuhakikishia usalama wa chanjo hizo kwa watoto.

About Author

Advertisement

 
Top