Na. Ahmad Mmow, Ruangwa-Lindi.
Muda mfupi tu tangu kusajiliwa na kuonesha mafanikio,wanachama wa chama cha msingi cha LIEMBA, kilichopo wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wameanza kuvurugana. Baada ya baadhi ya watu kutuhumu uongozi wa chama hicho kufanya ubadhirifu.

Wakizungumza na mtandao huu wanachama hao walidai kuwa mapendekezo yaliyotolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa mkoa Lindi, wakulima wangelipwa ya maajali(bonasi) shilingi 300/- kwa kila kilomoja, baada ya kukiuzia korosho chama hicho katika msimu wa 2014/2015. Hata hivyo wakulima walilipwa shilingi 270/-, kitendo ambacho hawakubaliani nacho.
Rashid Nkumbachile, aliyejitambulisha kuwa ni mwenyekiti wa kamati ya wakulima inayofanya ufuatiliaji wa malipo hayo. .Alisema malipo yaliyotarajiwa yalikuwa shilingi 300 kwa kila kilo moja hata hivyo wamelipwa shilingi 270 kwa kila kilomoja. Kitendo ambacho kinawapa mashaka kuwa shilingi 30/- wameibiwa na viongozi wao.
Alisema kutokana na mashaka hayo, serikali ya kijiji cha Liugulu, iliitisha mkutano ili kujadili utata uliojitokeza. Ndipo ilipoundwa kamati ya kufatilia zilipo shilingi 30 za kila kilo moja.
"Mashaka nikwamba nyaraka zilizopo zinaelekeza tungelipwa shilingi 300/-, dhamira yetu nikujua hiyo shilingi 30/- wapi ilipo, sasa tunafuatilia kwa katibu tawala wa mkoa ilitujue uhalali wa malipo hayo,"alisema Nkumbanjile.
Katibu wa kamati hiyo, Nandule Mayele, alisema wakulima waliokiuzia korosho chama hicho, msimu uliopita ni zaidi ya 600. ambao waliuza kilo 796150. Hivyo hawapotayari kuona shilingi 30 ya kila kilomoja kwa kilo hizo zimeingia kwa wajanja wachache.
Naye mjumbe wakamati hiyo, Omari Chijenja. Alisema wakulima hawakubali kulipwa kinyume cha mapendekezo waliyoahidiwa. Alisema wakulima na chama wanatakiwa kuwa na mawasiliano mazuri na wakulima ili kuwajengea imani. Vinginevyo chama hicho kitakufa kwani wakulima hawatakuwa tayari kupeleka mazao kwenye chama hicho.
"kwakuzingatia ukweli huo, uliitishwa mkutano mkuu ilikujadili suala hili" nasasa tumepeleka kwa wakubwa mkoani ili waweze kutueleza uhalali wa malipo ya shilingi 270 badala ya 300," alisema.
Mwenyekiti wa chama hicho cha msingi cha ushirika cha LIEMBA, Omari Chembeja, alisema hakuna wizi wowote uliofanyika. Bali wapowatu wachache ambao kwa makusudi wanataka kukivuruga chama hicho kwa sababu zao binafsi na kuharibu sifa na mafanikio ya haraka yaliyopatikana. Alibanisha kwamba nikweli walitarajia wakulima wangelipwa shilingi 300/- kwa kila kilomoja.
Hata hivyo makisio hayo yalifanyika bila ya kuondoa fedha za kampuni ambayo ililipia korosho katika mnada wa 8. Hata hivyo haukupata, kutokana na kuchelewa kulipia. "jambo hili lipo wazi na nyaraka zipo, tuliporejesha fedha hizo shilingi 102,758,250/- ambazo zilirejeshwa kwa kampuni kutoka kwenye shilingi milioni 300.21 ambazo zilikuwa kwenye akaunti na ndizo tulizokadiria kuwalipa kiasi wanachokisema,"alisema.
Alisema kabla hawajaanza kuwalipa wakulima walipata barua iliyowataka warejeshe pesa za kampuni kwani hazikuwa za chama. Ndipo makisio ya malipo ya awali yalipopungua nakusabisha wakulima walipwe shilingi 27O badala ya 300.
Alipoulizwa mrajisi msaidizi wa ushirika mkoa wa Lindi, Said Munjai alikiri kuwepo malalamiko hayo. Hata hivyo hakuwa tayari kuingia kwa undani kwa madai kuwa msemaji ni katibu tawala wa mkoa (RAS),
"Nikweli hata hayo maelezo hayo ya mwenyekiti wa chama ni yakweli, lakini mimi siyo msemaji ebu wasiliana na RAS,"alisema Munjai.
Juhudi za kumpata RAS wa Lindi, Abdallah Chikota hazizaa matunda kutokana na kuwa safarini kikazi. Hata hivyo uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa nikweli chama hicho kilirejesha fedha kwa kampuni ya Export Trading, shilingi 102.75 milioni. Kutokana na maagizo ya kamati ya muda ya chama kikuu cha ushirika cha RUNALI. Kupitia barua ya tarehe 24 jaunuari, mwaka huu. Iliyoagiza chama hicho kirejeshe kiasi hicho cha fedha kwa kampuni hiyo.
Lakini pia barua ya tarehe 4 ya mwezi mei mwaka huu toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi yenye kumbu namba JC.55/221/II/103, iliyosainiwa na Said Munjai, kwenda kwa afisa mtendaji wa kijiji cha Liugulu, ofisi hiyo imekiri kuwa upungufu wa malipo kwa wakulima ulisababishwa na chama hicho kurejesha fedha za kampuni ya Export. Nakwamba makisio yakulipwa wakulima shilingi 300 yalifanyika kabla ya fedha hizo kurejeshwa.
Lakini pia barua ya tarehe 4 ya mwezi mei mwaka huu toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi yenye kumbu namba JC.55/221/II/103, iliyosainiwa na Said Munjai, kwenda kwa afisa mtendaji wa kijiji cha Liugulu, ofisi hiyo imekiri kuwa upungufu wa malipo kwa wakulima ulisababishwa na chama hicho kurejesha fedha za kampuni ya Export. Nakwamba makisio yakulipwa wakulima shilingi 300 yalifanyika kabla ya fedha hizo kurejeshwa.
Chama cha msingi cha ushirika cha Liemba ni miongoni mwa vyama vichache vilivyopata mafanikio ya haraka. Kwani tangu kisajiliwe na kuanza biashara mwaka jana, kimeweza kununua trekta yenye thamani ya shilingi 53 milioni.