CCM YATAHADHARISHWA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MTAMA.

Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Baadhi ya wananchi katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, wamekitahadharisha Chama Cha Mapinduzi kuwa makini katika uteuzi wa mgombea ubunge wa jimbo hilo atakaye pitia chama hicho, huku baadhi yao wakiweka wazi kuwa kama chama hicho kitamteua mtu ambaye hakubaliki na wapiga kura hawatasita kumpigia mgombea wa chama cha upinzani.
Jimbo la Mtama
Wakizungumza na Lindiyetu.com katika jimbo la Mtama wiki hii, wananchi hao walisema tabia ya wananchi kupelekewa wagombea wasiowataka imekuwa ikikigharimu chama hicho. Juma Chileu aliyejitambulisha kuwa nimwanachama wa CUF, alisema ingwawa yeye sio mwanachama wa CCM lakini anajua kwamba wananchi wa jimbo hilo waliowengi wanamtu wanamuunga mkono bila kujali tofauti za vyama na mtu huyo ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Bila kumtaja ninani, Chileu alisema chama hicho kikifanya makosa na kumpitisha mtu ambaye sio chaguo la wananchi itakuwa neema kwa vyama vya upinzani hasa UKAWA.

Alisema wananchi wa sasa siokama wazamani ambao walikuwa watiifu kwa chama kiasi cha kutii maagizo hata yasiyo nafaida kwao. "wajiangalie sana na utaratibu wao, tabia ya kuwafanya wananchi kama makopo ya bafuni ambayo hajui maji machafu na masafi itawagharimu wasipobadilika," alionya Chileu. 

Jalasi Millanzi alisema ingawa yeye sio mwana CCM lakini anajua upepo unaelekea wapi na atapiga kura kwa kuangalia uwezo wa mgombea katika kuwaongoza nasiyo chama anachopitia. Alisema katika jimbo hilo wanaungana bila kujali tofauti za vyama kumpigia kura mtu ambaye yupo karibu na wananchi na ambaye ameanza kutoa ushirikiano nao kabla ya harakati za uchaguzi.

Hata hivyo kama CCM kitampitisha mtu tofauti na wanayemtaka basi watageukia upande mwingine (UKAWA) ambao alisema kuna mtu anatajwa kutaka kugombea na anazo sifa njema. "hili la kupigia mpira kwenye michongoma litakuwepo kama CCM watampitisha mtu asiyekubalika na wananchi. Wana CCM wenyewe wanasema watafanya kama walivyofanya watu wa Lindi mjini uchaguzi uliopita," alisema Jalasi.

Taji Shabani alisema katika jimbo hilo yanatajwa majina mengi ya wataogombea lakini wanawajua watu wakupigia kura. Alisema wapo ambao wameonesha ushirikiano katika kuchangia miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wakituo cha polisi cha Mtama, shule na misaada mingine. "mtu kama huyo lisipopitishwa jina lake tubaki kumpigia mgombea wa CCM kwa manufaa ya nan," alihoji Taji.

Hata hivyo Abdul Natosya alikuwa na maoni tofauti. Yeye alisema ataheshimu maamuzi ya chama nakwamba atampigia kura yule atayeteuliwa na Chama. Abdul alibainisha kuwa kundi linalotishia kupigia upinzani nila vijana ambao sio wanachama wa chama hicho na wengine sio wanachama wa chama chochote cha siasa. Kwani wana CCM wengi hawana mawazo
ya kukisaliti chama chao.

Katika jimbo hilo majina ya wanachama wawili wa Chama Cha Mapinduzi yanatajwa kutaka kuomba ridhaa ya chama hicho ili kugombea ubunge wa jimbo hilo. Majina ya makada hao ambao taarifa zinaeleza kuwa tayari wamejiandikisha kwenye daftari la kupigia kura kwenye jimbo hilo, ni katibu wa idara ya itikadi na uenezi wa CCM(T) Nape Nnauye, na kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) wilaya ya Lindi, ambaye pia ni diwani wa kata ya Vijibweni, Seleman Methew.

Ingawa hakuna hata mmoja kati yao aliyethibitisha wala kutangaza nia kama atawania nafasi hiyo.
Previous Post Next Post