Unknown Unknown Author
Title: HATIMAE MGOGORO WA MADEREVA NCHINI UMEMALIZIKA KWA TAMKO HILI LA SERIKALI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo jijini D...

Madareva
Mwenyekiti wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo jijini Dar es salaam ili kuwajulisha madereva wote nchini kuwa mwaka huu wamekubaliana na Mamlaka husika kuwa hakutakuwa na mafunzo kama ilivyoelezwa hapo awali. Kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.


Na Pius Yalula-MAELEZO-Dar es salaamSerikali imesema hakutakuwa na mafunzo kwa madereva wa malori na mabasi na wala hawatakiwi kwenda kusoma kozi fupi ili kuhuisha leseni zao kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali na kusababisha mgomo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga wakati akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam.

Alisema kuwa madereva wenye daraja E, C, C1, C2 na C3 walitakiwa kupata mafunzo ya muda mfupi kila baada ya miaka 3 kulingana na kanuni ziliandaliwa mwaka 2014 kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Chuo cha Taifa ya Usafishaji(NIT), Vyama vya Madereva, Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali na Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo Tanzania (TATOA), lakini kwa mwaka huu hawatatekeleza kanuni hiyo.

Kamanda Mpinga alisisitiza kuwa kanuni hiyo haitatumika mwaka huu badala yake madereva wataendelea na utaratibu wao wa zamani wa kubadilisha na kuhuisha leseni zao kwa zile ambazo zitakuwa zimekwisha bila kuulizwa vyeti.

Aliongeza kuwa hadi hivi sasa mitala ya mafunzo hayo ya muda mfupi bado haijakamilika na wala Serikali haijawahi kupanga ada za mafunzo hayo, kwa hiyo utaratibu wa zamani utaendelea kutumika kama ulivyokuwa hapo awali.

Kamanda Mpinga alitoa wito kwa madereva wote kuwa wavumilivu kwa matatizo yao wakati Kamati ya kudumu ya kutatua matatizo ya sekta ya usafishaji ikendelea kuyatafutia ufumbuzi.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi na wasafiri kutoa taarifa kwa viongozi wa Jeshi hilo endapo wanaona Askari wao au dereva anatenda vitendo visivyo vya kimaadili ili aweze kuchukuliwa hatua.

Alisema kuwa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kipo wakati tayari kupokea malalamiko ya kuyachukulia hatua ili kulinda maisha ya wasafiri na mali zao, hivyo ni vizuri wakaripoti wale wote wanaohatarisha maisha ya wenzao.

About Author

Advertisement

 
Top