MABOMU YARINDIMA NACHINGWEA,MADUKA YAFUNGWA KWA MASAA KADHAA.

Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Mji wa Nachingwea jana ulishuhudia vurugu kwa mara nyingine, wakati polisi walipopambana na waendesha pikipiki za abiria (bodaboda).
vurugu nachingwea
Picha kutoka Maktaba

Taarifa kutoka mjini humo zinaeleza kuwa vurugu hizo ambazo zilisababisha maduka hasa yaliyo maeneo ya sokoni na kituo cha mabasi zilizodumu kwa takribani saa sita. Zimeelezwa kuwa zilitokana na waendesha pikipiki kutokubali kitendo cha polisi kumkamata mwenzao usiku akiwa nyumbani kwake. Kosa likielezwa alipakia zaidi ya abiria mmoja.

Mashuhuda waliozungumza na Lindiyetu.com, wameleza kuwa waendesha pikipiki hao walianza kuhamaki baada ya mwenzao kuhukumiwa adhabu ya kifungo gerezani. Mashuhuda hao ikiwamo baadhi ya waendesha pikipiki walisema kitendo cha kumuendea mwendesha pikipiki usiku kwa kosa hilo na kuhumiwa kifungo ni cha uonevu. Hivyo waliamua kwenda kwa askari ambaye alihusika na uonevu ili nae wamuadhibu.
"mwandishi wanaosababisha vurugu ni polisi wala sio raia,iweje kosa la kupakia zaidi ya abiria mmoja waende kumfungulisha na kumkamata usiku wa manane tena nikosa ambalo angefainiwa lakini amefungwa miezi sita jela ni uonevu,"alilalamika mwendesha pikipiki.

Mmoja wa mashuhuda alisema hali ilikuwa mbaya kuanzia mahakamani baada ya mahakama kumuhukumu mwendesha pikipiki mwenzao ambapo vijana hao waliandamana kwenda mtaa wa Kilimanihewa, mahali ambako zipo nyumba za polisi.
"ndipo vurugu zilipoanza na kuenea kwakasi wakati polisi walipojaribu kuwatawanya waendesha pikipiki na vijana wengine ambao walikuwa wanachoma magurudumu(matairi) ya gari" polisi nao wakijaribu kujihami na kuwatanya kwa mabomu ya machozi," alisema shuhuda huyo.

Mmoja wa madereva wa magari ya kusafirisha abiria kati ya Nachingwea na Lindi aliuambia mtandao huu kwamba alilazimika kushusha abari katika mtaa wa Kilimani hewa baada ya kushindwa kufika na kuingia kituo cha mabasi cha Nachingwea. Alisema alichukua uamuzi huo baada ya barabara kufungwa na umati wa watu ambao wengine walikuwa wanakimbia huku na kule na wakati moshi mzito uliotokana na kuchomwa matairi na mobomu ukiwa umetanda. "kwakawaida huwa tunaingia saba pale Nachingwea,lakini tuliambiwa vurugu zilianza saa sita na tuliendelea kushuhudia zikiendelea hadi jioni" soko na maduka yalifungwa,hali ilikuwa nimbaya sana hasa maeneo ya kati ya mj," alisema.

Juhudi za kuwapata viongozi wa umoja wa endesha pikipiki na teksi wa Nachingwea hazikufanikiwa baada ya simu zao kutokuwa hewani kipindi chote. Lakini pia juhudi za kumpata kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi iliathibitishe au kukanusha taarifa hizi hazikuzaa matunda ambaye pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi hakujibu.
Previous Post Next Post