Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Arusha,Feruz Bano akimkabidhi kitabu cha kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea aliyetangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute jana ofisini kwake mara alipofika kujitambulisha na kutangaza nia.
Mgombea aliyetangaza kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa chama hicho wilayani Arusha jana alipofika kujitambulisha na kutangaza nia.
(picha na moses mashalla)
Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Arusha kimetoa onyo kwa wagombea waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho kuacha tabia ya kuchafuana na kuanza kampeni kabla ya muda.
Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha, Ferooz Bano wakati akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho, Kim Fute.
Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani humo kujitambulisha na kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.
Hadi sasa jumla ya wagombea saba ambao ni Kim Fute, Phillemon Mollel "Monaban”, Mustapha Panju "Bushbuck”, Victor Njau, David Rwenyagira, Deo Mtui, Francis Laiser pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini, Felix Mrema wamejitokeza kutia nia kuwania jimbo la Arusha mjini.
Akizungumza mara baada kumkabidhi kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutia nia kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa wapiga kura.
“Muda wa kampeni bado haujafika hatutaki nyinyi wagombea muanze kuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano
Hatahivyo, kwa upande wake mgombea huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya chama hicho na kusisitiza kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini mkubwa.
Fute,alitangaza rasmi kuinga katika kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe la uongozi.