Viongozi na watumishi wa serikali, mkoani Lindi. Wametakiwa kujitenga na siasa katika kutekeleza majumu yao, bali wazingatie sheria, taratibu na miongozo ya serikali iliyomadarakani.
Wito huo umetolewa kwa nyakati na maeneo tofauti na kaimu katibu tawala wa mkoa wa Lindi, Abdul Dachi, alipotembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vya maabara za sekondari katika halmashauri za wilaya za Liwale, Nachingwea, Ruangwa, Lindi na manispaa ya Lindi.
Alisema viongozi na watendaji wa serikali ni watekelezaji wa mipango ya serikali, hivyo wasijiingize kwenye siasa au kuyumbushwa na wanasiasa nakusababisha mipango ya maendeleo kukwama bila sababu za msingi.
Dachi alibainisha kuwa watendaji wanatakiwa kuzipuuza kauli za baadhi ya wanasiasa, ambazo hazinamaslahi kwa taifa. Ikiwamo kuwachochea na kuwashawishi wananchi wasishiriki na kuchangia shuguli za maendeleo.
"sisi niwatumishi wa serikali tusijiingize na kushabikia mambo ya siasa, wapuuzeni wanasiasa wanataka kukwamisha kazi za maendeleo,"alisema Dachi.
Alisema ingawa ujenzi wa vyumba vya maabara unatakiwa kukamilika tarehe 3O mwezi juni mwaka huu, lakini viongozi na watumishi hao wahakikishe vyumba vya maabara vinavyo jengwa ni lazima viwe ubora unaolingana na fedha zinazotumika.
Aidha kaimu katibu tawala huyo ameagiza ujenzi huo uende sambamba na miundo mbinu ya kuvunia maji kwenye shule hizo ili punguza adha ya maji katika maeneo hayo.