Unknown Unknown Author
Title: TWIGA STARS YAFUZU MICHEZO YA AFRIKA, SASA KUKUTANA NA KONGO BRAZAVILLE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Michezo ya Afrika baada ya kuitoa Zambia, She-Polopolo ...
TIMU ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Michezo ya Afrika baada ya kuitoa Zambia, She-Polopolo kwa jumla ya mabao 6-5.

Katika mchezo wa marudiano uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Twiga inayofundishwa na Rogasian Kaijage imelala mabao 3-2, baada ya awali kushinda 4-2 nchini Zambia.

Mabao ya Twiga yalifungwa na Asha Rashid 'Mwalala' dakika ya tatu na Mwanahamisi Shurua 'Gaucho' dakika ya 29, wakati ya Zambia yamefungwa na Grace Chanda dakika ya 50, Irene Lungu dakika ya 61 kwa penalti baada ya Nahodha Sofia Mwasikili kuunawa mpira na la tatu Misozi Chisa dakika ya 90.

Twiga Stars
Wachezaji wa Twiga Stars wakishangilia moja ya mabao yao leo Uwanja wa Taifa

Twiga sasa itakwenda Kongo- Brazzavile Septemba mwaka huu kwenye AAG.

Kikosi cha Twiga Stars kilikuwa; Fatuma Omar, Anastas Katunzi, Stumai Abdalla, fatuma Makusanya, Fatuma Isa, Sophia Mwasikili, Donisia Daniel, Amina Ally, Shelder Boniface, Asha Rashid na Mwanahamisi Shurua.

Zambia; Hazel Natasha Nali, Rachel Nachula, Lweendo Chisamu, Joana Benai, Mary Mwakapila, Mary Wilomba, Misozi Chisa Rachel, Meya Banda, Annie Kibanjo, Grace Chanda na Barbra Banda.

>>BIN ZUBERY

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top