AJALI YA BASI LA ABIRIA NA LORI LA FUSO RUAHA MBUYUNI LEO
byUnknown-
0
Habari zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo kuteketea kwa moto maeneo ya milimani kilomita kadhaa kutoka Ruaha Mbuyuni kuelekea Morogoro, inasemekana abiria wengi walikuwa ni wanafunzi, ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi leo.
Pichani ni basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto.
Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana.
Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...