Unknown Unknown Author
Title: SHULE YAKOSA MATUNDU YA VYOO TANGU KUJENGWA KWAKE MIAKA YA 1960, LINDI VIJIJINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakati serikali ikiwa katika mpango mkakati wa kuwa na matokeo makubwa ya mipango yake ya maendeleo uliopewa jina la MATOKEO MAKUBWA SASA(...
Wakati serikali ikiwa katika mpango mkakati wa kuwa na matokeo makubwa ya mipango yake ya maendeleo uliopewa jina la MATOKEO MAKUBWA SASA(BRN), Kumekuwa na hali ya kukatisha tamaa kwa baada ya wizara zake kama zinaweza kutoa hayo matokeo makubwa.
Darasa
Miongoni mwa wizara hizo ni wizara ya elimu na mafunzo, ambapo baadhi ya shule hazina vyoo wala nyumba za waalimu tangu zianzishwe.

Hayo yamebainika katika kijiji cha Kilangala B, mkoani Lindi. Wakizungumza na waandishi wa habari waliokwenda kijijini hapo jana, baadhi ya wananchi na viongozi wa kijiji hicho walisema shule hiyo ya msingi yenye wanafunzi 559, tangu ianzishwe na kanisa katoliki miaka ya 196O haijawahi kuwa na vyoo vya kudumu na inanyumba moja tu ya waalimu.

Selina Mtamelo aliyejitambulisha ni mkazi wa kijiji hicho, alisema tatizo la vyoo katika shule hiyo ni sugu na serikali haioneshi kujali kutokana na kushindwa kuunga mkono juhudi za wananchi, ambao walichimba mashimo baada ya kuambiwa halmashauri ya wilaya itachangia pesa zitakazo tumika katika ujenzi wa vyoo hivyo hata hivyo haijatekeleza ahadi yake.

Juma Mwaka, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo. Alisema hali katika shule hiyo ni mbaya kwani wanafunzi 559 wanaosoma katika shule hiyo wanatumia choo kimoja cha muda,  ambacho kina tundu moja nakutumiwa na wanafunzi wakike na kiume hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi kujisaidia vichani.
"hali hiyo siyo kwa wanafunzi tu, bali hata waalimu wanapata shida sana. Hakuna choo cha waalimu, waalimu wote 11 wanajisaidia kwenye choo kimoja chenye tundu moja ambacho kipo kwenye nyumba ya mwalimu mkuu, nacho nicha muda.
"huwezi kuamini kama shule hii ipo barabarani, maana hata nyumba ya walimu ipo moja tu,wengine kumi wanaishi kwenye nyumba za kupanga," alisema Mwaka.Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho,

Nurudin Mohamed, Alisema halmashauri ya wilaya ya Lindi hiyo inatambua tatizo hilo. Bali sababu inayosababisha kushindwa kuliondoa kwa haraka ni lafedha.Kwani halmashauri bado haijapata fedha. Aliongeza kusema matatizo hayapo katika shule hiyo pekee bali shule nyingi zinaupungufu wa mambo ya msingi, lakini yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa fedha.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top