Unknown Unknown Author
Title: MGOMO WA MADEREVA:: SERIKALI KUPITIA MIKATABA YA MADEREVA NCHINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa kazi na ajira GAUDENTIA KABAKA amekutana na viongozi wa vyama vya vyombo vya usafiri ikiwemo malori, mabasi, taksi na pikipiki ...
Waziri wa kazi na ajira GAUDENTIA KABAKA amekutana na viongozi wa vyama vya vyombo vya usafiri ikiwemo malori, mabasi, taksi na pikipiki na kusema serikali itaanza kupitia mikataba ya ajira za madereva wa magari hapa nchini.

Waziri KABAKA amesema wadau hao wa usafiri wanatarajiwa kukutana tena tarehe 18 mwezi huu ambapo watakutana na mawaziri wa mambo ya ndani, kazi na ajira, uchukuzi na ujenzi ambapo kero mbalimbali za madereva zitazungumzwa na kutafutiwa ufumbuzi.

Wakati Waziri akiyasema hayo baadhi ya madereva wa mabasi yanayofanya biashara ya usafiri katika jiji la DSM na yale yanayokwenda nje ya jiji la DSM wamesema wanakutana jijini DSM kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mafunzo kwa madereva.

Madereva hao wamesema wanakutana kujadili pamoja na mambo mengine agizo linalowataka kwenda kozi ya kuboresha taaluma yao kila baada ya miaka mitatu.

TASWIRA YA MAPEMA LEO ASUBUHI
Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungu huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.
Ubungo mambo yalikuwa namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top