Unknown Unknown Author
Title: PENZI LA NAY NA SHAMSA LA SABABISHA VILIO KWA SIWEMA NA MUME WA SHAMSA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Penzi la staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford na Staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ limeibua tafrani kubwa huku walioku...
Penzi la staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford na Staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ limeibua tafrani kubwa huku waliokuwa wapenzi wa mastaa hao wakijikuta wakiangua vilio kweupe.
Nay na Shamsa
Kwa mujibu wa gazeti la Ijumaa, Mara baada ya wawili hao kutangazwa rasmi kuwa sasa ni mahaba niue huku picha za ushahidi zikimwagwa, aliyekuwa mwandani wa Nay, Siwema a.k.a Wemalicious na aliyekuwa mume wa Shamsa, Dickson ‘Dick’ wanadaiwa kujikuta kwenye hali mbaya kiasi cha kumwaga machozi.

Akizungumza na gazeti hilo kwa njia ya simu kutoka jijini Mwanza, Siwema mwenye mvuto wa kuvunja midume shingo alianika mazito kwamba, kitendo cha Nay kumuacha na muda si mrefu kwenda kwa Shamsa ni upuuzi.
Siwema alifunguka kwamba, kinachomshangaza ni kitendo cha Shamsa kuvaa nguo zake na kufanyia mazoezi.
Mwanamama huyo alisema watu watamtukana kwa kuwa hawajui tabia ya Nay kwani hata Shamsa atamshindwa tu.

“Nilivumilia vitu vingi sana. Maumivu nayajua mimi, nyumba tuliyojenga wote, anaingia mwanamke mwingine. Namhurumia sana Shamsa kwani hajui tabia za Nay,” alifunguka mtoto mweupe, Siwema kwa uchungu.

Habari zilieleza kwamba, Siwema alijua muda mrefu kuwa Nay anatembea na Shamsa lakini alipomuuliza staa huyo anayetamba na Ngoma ya Akadumba alimwambia walishaachana.

Akizungumzia ishu hiyo, Nay alisema kuwa yeye yupo na Shamsa na kwamba anamshangaa huyo Siwema kwani alishaachana naye.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti hilo, naye kama Siwema, baada ya penzi la Shamsa na Nay kuwa ndiyo habari ya mjini huku wakitupia picha za malovee mtandaoni, mume wa Shamsa, Dick alipaniki kiasi cha kutokwa machozi huku akitafuta namna ya kupooza machungu.

Habari zilidai kwamba, Dick alikimbilia kwa staa wa sinema za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’ na kwenda kumuomba aokoe jahazi akimshitakia Shamsa kuwa ameamua kumwacha na kuamua kutembea na Nay, jambo ambalo analiona kuwa ni udhalilishaji kwani ni mkewe ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Terry.

Ilidaiwa kuwa, baada ya Dick kufika nyumbani kwa JB maeneo ya Ubungo-Kibangu, Dar na kumweleza hayo, mwigizaji huyo alimpigia simu Shamsa ambaye humwita Daddy na kumuuliza juu ya suala hilo ambapo alimweleza kuwa alishaachana na Dick hivyo kila mmoja ana maisha yake.
Katika hali hiyo, JB aliwataka kukaa chini na kuyamaliza kiutu uzima kuliko kuwekeana kinyongo.

Baada ya kusikia kilichopo upande wa mume wa Shamsa, gazeti hilolilimgeukia Shamsa na kumwelezea kila kitu kilichopo ambapo alionesha kumshangaa Dick kwa kuwa alishamalizana naye tangu Oktoba, mwaka jana.
“Kwanza namshangaa kwa nini anawaka wakati kila mtu ana maisha yake?“Tulishaachana tangu mwaka jana so kila mtu ana maisha yake,” alisema Shamsa ambaye kwa sasa amehamishia moyo wake kwa Nay.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top