Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema vifo vya watanzania watatu vilivyotokea nchni humo havina mahusiano na mauaji hayo ZENOPHOBIA na kusisitiza serikali ya afrika kusini imeanza kuchukua hatua na tayari watu wawatu waliohusika na kifo cha rais wa msumbiji wamekamatwa.
Akizungumzia idadi ya watanzania waliohifadhiwa kwenye kambi katika mji wa DURBUN, Mhe Membe amesema takribani watanzania 23 wamehifadhiwa katika kambi ya isipingo iliyo na zaidi ya raia wa kigeni elfu tatu ambao wako chini ya ulinzi wa serikali ya afrika kusini na kusisitiza serikali imeanza utaratibu wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati yao.
Akielezea msimamo wa tanzania kufuatia mauaji hayo ya ZENOPHOBIA yanayoendelea nchni afrika kusini, Mhe. Membe amesema serikali inaunga na jumuiya ya nchi za SADC kulaani vitendo vya mauaji yanayoendelea nchni humo ambapo watu 8 wamekwisha uawa kikatili na kuita serikali ya afrika kusini kuzuia mauaji hayo haraka iwezekanavyo.
Aidha amesema serikali ya Tanzania haitakuwa na tatizo la watanzania kurudi nchni humo baada ya mauaji kudhibitiwa na kwa upande wa wafanyabishara walisajiliwa kihalali na kupoteza mali zao, serikali itawasiliana na wanasheria wake ili kuona namna ya kutafuta namna ya nchi hiyo kuwafidia hasara waliyoipata.