Unknown Unknown Author
Title: CCM ZANZIBAR YAMFUKUZA UANACHAMA MZEE HASSAN NASSOR MOYO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mzee HASSAN NASSOR MOYO Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa mjini Magharibi kisiwani Unguja huko Zanzibar imemfukuza uan...
HASSAN NASSOR MOYO
Mzee HASSAN NASSOR MOYO

Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa mjini Magharibi kisiwani Unguja huko Zanzibar imemfukuza uanachama wa chama hicho Mzee HASSAN NASSOR MOYO baaya ya kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mjini Unguja Katibu wa CCM mkoa wa mjini Magharibi AZIZA RAMADHANI MAPURI amesema maamuzi hayo yamekuja baada ya MZEE HASSAN NASSOR MOYO kuonekana kwenda kinyume na maadili ya chama kwa mujibu wa muongozo wa Katiba ya Chama cha Mapinduzi.

Hata hivyo katibu huyo wa ccm mkoa wa mjini magharibi, amesema endapo Mzee MOYO hataridhika na uamuzi huo ana haki ya kikatiba ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika ngazi kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi ambayo itaweza kusikilzia shauri lake na kulitolea uamuzi wa mwisho.

About Author

Advertisement

 
Top