Unknown Unknown Author
Title: MABASI MAWILI YAGONGANA USO KWA USO LEO MAENEO YA MKATA MKOANI TANGA, WATU 10 WAPOTEZA MAISHA 32 WAPATA MAJERUHI MAKUBWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watu 10 wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira y...
Watu 10 wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.
ajali
Akizungumza na Mwandishi wetu Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda, gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.

Baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.
ajali
Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.
ajali
 Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
ajali
 Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top