Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe
Rais Mugabe ametoa mwito huo wakati akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa viongozi Vijana kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika na China unaofanyika katika ukumbi wa mikotano wa Ngurdoto nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo Rais Mugabe ametumia muda mwingi kuwaasa na kutoa mwito kwa viongozi hao vijana akisistiza kuwa Bara la Afrika linategemea mchango wa Fikra zinazojali uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu katika utumishi.
Awali akizungumza katika Mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete ameonyesha imani aliyoanayo kupitia mkutano wa viongozi vijana kutoka Afrika na Uchina kwamba utatoa fursa ya kutoka na maazimio yatakayokuwa na tija kwa mustakabali wa watu wote.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.